Na Lucy Lyatuu
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke iinatarajiwa kufanyiwa maboresho katika maeneo ya huduma Kwa wateja na kuondoka changamoto ya Mawasiliano kutola Kitengo li Moja kwenda kingine.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya John Jingu amesema hayo leo alipotembelea Hospitalini hapo kuangalia u ora wa utoaji huduma na kuongeza kuwa maboresho hayo yatasaidia huduma iwe rahisi na yenye tija.
Amesema wamekutana na wagonjwa kuona ni namna gani wanapokea huduma ambapo kiwango kikubwa wagonjwa wanasema wanaridhika na huduma zinazotolewa .
” Katika uboreshaji huo kuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa ufanisi lakini kwa tija zaidi eneo la huduma kwa wateja inanatakiwa mtu akifika Hospitalini hapa aweze kupata huduma mara moja na asikae zaidi ya muda unaohitajika kukaa,” amesema.
Amesema kuna changamoto zingine za mawasiliano kutoka kitengo kimoja kwenda kingine na yenyewe inaweza kuleta ucheleweshaji wa hapa na pale lakini Serikali inawekeza kwa kiwango kikubwa kwenye tehama Ili kusaidia kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji .
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Joseph Kimaro amesema ziara hiyo inawapa motisha wao watumishi walio chini ya Wizara ya Afya ili waweze kuendelea kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wanaozitegemea.