MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Hakuna Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi Kwa Watumishi Wapya Wa Umma Kwa Sasa -Kikwete
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Hakuna Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi Kwa Watumishi Wapya Wa Umma Kwa Sasa -Kikwete
Habari

Hakuna Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi Kwa Watumishi Wapya Wa Umma Kwa Sasa -Kikwete

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu, Dodoma
SERIKALI  imewataka watumishi wa umma wapya waliopata ajira kwa mwaka 2026  na kupangiwa vituo vyao vya kazi kutambua kuwa  kwa sasa  hakutokuwa na mabadiliko ya vituo vyao vya kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Ridhiwan Kikwete, amesema  hayo jijini hapa wakati akielezea  utekelezaji wa maelekwzo ya Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha siku 100  tangu alipoingia madarakani.
Kikwete amesema  kwa sasa Serikali haitafanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa watumishi wa umma kwa kuwa  mpangilio wa nafasi hizo ni kwa mujibu wa mgawango wa eneo husika.
Amesema na kwa watumishi ambao hawataripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu kupata barua nafasi zao zinaweza kuchukuliwa na wengine ambao walibakia katika kanzidata.
Kikwete amewataka waajiri pia wanapowapokea watumishi hao kutoa taarifa zao kwa Mhariri mkuu wa gazeti la serikali ili kutambuliwa.
‎
” Yapo  maombi mengi kutoka kwa watumishi wakiomna nafasibalimbali za kazi lakinibpia yapo maombi ya kubadilishwa vituo vya kazi,  maombi hayo hayawezi kufanyiwa kazi kwa sasa, ” amesema Waziri Kikwete
‎
Amebainisha kuwa nafasi zote za kazi zilitolewa kwa kuzingatia uhitaji wa kila Halmashauri au mwajiri husika, hivyo kufanya mabadiliko ya vituo vya kazi kungepunguza idadi ya watumishi waliopangwa katika maeneo husika na kuathiri mgawanyiko uliopangwa na Serikali.
Aliongeza kuwa katika siku 100 tangu Rais Dkt Samia kuingia madarakani tayari watumishi wapya 12,000 wamepata ajira wakiwemo wa kada ya afya 5000 na elimu 7000.
Kikwete amesema watumishi wapya 735 walioripoti katika vituo vyao vya kazi kabla ya kufungwa kwa mfumo wa mishahara  tayari wamepewa mishahara kwa kuwa waliripoti kabla na kwamba watumishi  wote wataingizwa kwenye mfumo wa mshahara kadri walivyoripoti katika vituo vyao.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali ina mpango wa kutoa ajira nyingine 41,500 katika kada mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, kilimo, uvuvi, uhandisi, zimamoto na hata polisi na kuwaomba wananchi kuendelea kutumia mfumo wa kuomba ajira ili kipindi zikitangazwa waweze kuwa miongoni mwa watakaochukuliwa.
Katika hatua nyingine Kikwete amesema katika kipindi cha siku 100,Wizara eanzisha mfumo wa uwajibikaji ili viongozi wa umma kuzungumza na wananchi moja kwa moja ili kujibu maswali na malalamiko yao.
” Mfumo huu ni rafiki “Sema na Kiongozi”ni Mfumo wa kielekteoniki umeundwa kupokea malalamiko lengo likiwa ni kuimarisha  utawala bora na viongozi wanaohusika wanaanzia ngazi ya wilaya na mkoa na kwamba wananchi wanaweza kuwasilisha malalamiko yao na sauti zao kusikilizwa na kutolewa maamuzi, ” Amesema.

You Might Also Like

Umoja, Mshikamano Vyatawala Mkutano Wa SADC

Trump Amteua Mtendaji Mkuu White House, Safari Ya Kuunda Timu Yake

REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani

Watafiti Mradi Wa  AGRISPAK kutoka SUA Waanza Uandaaji Wa Vitabu Vidogo

VETA Yapaa Miaka Minne Ya Rais Samia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Bunge Bonanza 2026 Kuikutanisha Simba Na Yanga Dodoma
Next Article Jafo Ahoji Fedha Za Ujenzi Barabara Ya Mzenga – Kisarawe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?