MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: GWSON yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa,mgongo wazi kumbukizi ya Mwl.Nyerere
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > GWSON yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa,mgongo wazi kumbukizi ya Mwl.Nyerere
Uncategorized

GWSON yawakumbuka watoto wenye vichwa vikubwa,mgongo wazi kumbukizi ya Mwl.Nyerere

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
KIKUNDI cha Wanawake waishio Goba(GWSON)kimetoa msaada wa vifaa tiba kwa Watoto wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI).
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa msaada huo,Mkurugenzi wa GWSON Marietha Kaole alisema msaada huo ni nyenzo muhimu katika kusaidia kundi hilo la watoto katika hospitali hiyo.
Amesema ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuhakikisha wanalinda na kutunza maisha ya wagonjwa kwa kuhakikisha wanawajali na kuwashika mkono.
” Tumeona kuna uhitaji mkubwa wa vifaa tiba kwa watoto hao wa vichwa vikubwa na mgongo wazi,hivyo tukaona ni vema kuja kutoa msaada huu katika kumbukizi ya Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Nyerere na kumbukizi ya kuanzishwa kwa umoja wetu ambapo umefikia miaka mitatu hadi sasa,”amesema na kuongeza
”Hii sio mara ya kwanza katika kutoa msaada huu tayari tumetembelea hospitali ya Ocean Road,Tumetoa msaada wa huduma za matibabu kwa watu mbalimbali kupima bure magonjwa ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi ,Matiti pamoja na Tezi Dume kwa wakazi wa Goba,”amesema.
 
Amesema GWSON ni kikundi cha wanawake walioamua kushirikiana
katika kusaidiana kiuchumi na kijamii na kugusa wahitaji wale wadogo zaidi waliosahaulika katika jamii.
”Katika kikundi chetu kinaongozwa na kauli mbiu ya Mwanamke Jitambue ambayo imebeba maono ya Mwalimu Nyerere ya Kupinga Vita Adui,Ujinga,Maradhi na Umaskini,”amesema.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho,Salma Magesa amesema mbali na vifaa tiba pia wametoa mahitaji mengine kwa watoto hao kama Maji,Nguo,Pampers na Taulo za kike.
Amesema bado uhitaji wa vifaa mbalimbali kwa watoto hao unahitajika hivyo jamii iendelee kujitoa na kuwakumbuka katika kuwasaidia ili waweze kufarijika.
”Tumeguswa na jamii hasa watoto hawa ambapo  tumejichangisha fedha  kidogo na kuamua kuwaletea Dawa,maji,Taulo za Kike,Pampares,Nguo na hii ndio dhamira ya kuanzishwa kwa Kikundi hichi ambapo tuliamua kuisaidia jamii iliyotuzunguka,”amesema
Naye Afisa Ustawi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI),Sophia Nassoni amewashukuru kikundi hicho kwa kutoa msaada huo kwa watoto hao hiyo inaonyesha ishara ya upendo mkubwa kwa watoto hao.
Amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa tiba hivyo ambapo kwa mwaka wanawafanyia upasuaji  watoto hao 600 hadi 900 huku kwa watoto 1000 wanaozaliwa,watoto wanne hadi sita  wanazaliwa na ulemavu huo.
Ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwasaidie watu hao na kutowaacha watu hao kwani wanauhitaji vitu mbalimbali ikiwemo Vitimwendo,Dawa na mrija wa punguza maji kwenye kichwa.

You Might Also Like

Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Wasira akipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kwa kuenzi Falsafa za Baba wa Taifa

Rais Mwinyi aipongeza Airpay kudhamini tamasha la fahari ya Zanzibar, kusaidia wananchi kupata mikopo kidigitali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini
Next Article Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

JAB Yatoa Mwezi Moja Kuthibitishwa, kupewa vitabulisho
Habari May 22, 2025
Hali Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mipaka Ni Salama
Habari May 22, 2025
Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati
Habari May 22, 2025
Aloe Dorotheae, Mmea Unaopatikana Tanzania Pekee
Habari May 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?