Na Danson Kaijage
TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imepata mafanikio makubwa katika serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Nokta Banteze amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha uongozi wa Rais Samia.
Amesema kutokana na tafiti zinazofanywa na GST, zimewezesha kuchangia sehemu kubwa ya mnyororo wa uchumi kwa kusababisha kuanzishwa kwa migodi mingi.

Pia amesema GST ina maabara ya kisasa inayotoa huduma za uchunguzi wa madini kwenye sampuli za miamba, udongo, maji na mimea.
Amesema maabara hiyo ni kubwa na ya kipekee ya Serikali, inaendeshwa kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.
Ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni kuongezeka kwa makusanyo ya ndani kutoka wastani wa Sh. Bilioni 1.2 mwaka 2021 hadi Sh. Bilioni 2.3 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32.

Pia kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazochunguzwa kutoka wastani wa sampuli 19,184 mwaka 2021 hadi sampuli 25,793 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 34.45.
“Ongezeko hili limetokana na maboresho makubwa ya maabara yaliyofanyika hasa katika ununuzi wa vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi wa sampuli,” amesema.
Vile vile kuongezeka kwa bajeti ya taasisi kutoka wastani wa Sh.Bilioni 10 mwaka 2021/2022 hadi Sh. Bilioni 110 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 1,000 kwa ajili ya kukamilisha majukumu mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.
“