Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA ya Dawa Za Kulevya Nchini (DCEA) imesema Iko kwenyeboperesheninmaalum kuhakikisha wanatoka elimu maalum kwa nchi mzima kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo Ili kujua aina ya Dawa za Kulevya na kwamba wakikamatwa na dawa hizo Sheria inasema nini.
Kamisha Wa Mamlaka hiyo Areta Lyimo amesema hayo katika Banda la Mamlaka hiyo lililoko katika maonesho ya 49 ya Biashara ya kimaraifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema pamoja na elimu hiyo kwa makundi hayo lakini pia wanafanya operesheni maalum ya kukamata wale wote ambao bado wanaendelea kujihusisha na biashara ya usambazaji na uzalishajibwa dawa hizo lengo likiwa ni kuhakikisha KWAMBA ndani ya kipindi kifupi wanamaliza kabisa tatizo la dawa za Kulevya zinazoingia nchini.

Amesema Kwa Kufanya hivyo itasaidia wale wanafanya biashara hizo kuacha na wale ambao hawajaingia wasiingie na wale ambao tayari kufahanu vituo vya huduma kwa kuwa serikali inatola huduma bure kwa wale walioatgirika,lengo likiwa ni wananchi wote kurudi kwenye mfumo wakiwa na afya njema Ili kuungana kwa pamoja kujenga Uchumi wa nchi.
Kuhusu Hali ya Dawa za Kulevya Nchini amesema Hali inaendelea kuimarika kutokana na operesheni mbalimbali ambazo zimefanywa.
“Hadi sasa kuna baadhinya dawa kama heroine,methanoine na cocaine zimeadimika na kupungua sana nchini na hata kwenye vijiwe na maeneo mbalimbali hakuna waraibu na Wateja wanaokuwa kwenye vituo vya mabasi wakininginia,..Hali ni tofauti,” amesema na kuongeza kuwa hiyo ni kutokana na serikali kuwachukua waraibu kuwa peleka kwenye vituo vya Tiba wakiendelea Kupata huduma bure.