Na Mwandishi Wetu
LEO Julai mosi, 2025 Dkt. Semistatus Mashimba amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua inayoashiria mwanzo rasmi wa safari yake ya kisiasa kuelekea kulitumikia jimbo hilo kwa nafasi ya juu ya uongozi, huku akionyesha dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Busega kupitia uzoefu na uadilifu alioujenga katika nafasi mbalimbali alizowahi kushika.