Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa biashara kwa saa 24 zitaanza kufanyika Februari 22, mwaka huu 2025.
Chalamila amezungumza hayo Januari 30, 2025 alipokutana na Waandishi wa Habari kwa ajili ya kushukuru kwa mkutano mkubwa wa nishati uluomalizika hivi karibuni Mkoani Dar es Salaam.
” Katika kueleka kufungua zaidi Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kushirikiana na watendaji wenzangu tumekubaliana kuwa Dar es Salaam ianze kujipanga kufanya biashara saa 24.
“Februari 22 mwaka huu, itakuwa ni siku maalum ya kuzindua utaratibu wa kuanza rasmi kufanya biashara usiku,” amesema.
Ametaja eneo litakalozinduliwa nila kwenye viunga vyote vya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kuelekea Kariakoo.
Amesema eneo love hilo litakuwa na na utaratibu maalum kwamba biashara gani itakuwa wapi.
” Kwa mfano vyakula vitakuwa eneo gani, vinywaji eneo lipi. Pia kutakuwa na ufungaji wa baadhi za barabara kuingia Kariakoo kwa siku tuliyokubaliana ya uzinduzi,” amesema.
Amesema uzinduzi huo ulipangwa ufanyike Januari name, lakini kuna baadhi ya maeneo muhimu hayajawekwa taa.