Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekabidhi Sh. Milioni 100 alizoahidi kwa wakazi wa Saranga Wilaya ya Ubungo, kutekeleza ahadi yake aliyoitoa katika ziara aliyoifanya.
Chalamila amekabidhi fedha hizo ili kukamilisha ujenzi kwani eneo hilo kuna changamoto ya Zahanati kwa kipindi kirefu licha ya kuwa na wakazi wengi wanaohitaji huduma ya Afya.

Vilevile Chalamila amekabidhi mifuko ya Saruji ili ujenzi wa zahanati hiyo uanze mara moja kwa kuwa tayari jengo hilo lilishaanza kujengwa kinachotakiwa kufanyika ni ukamilishaji wake ili lifikie hatua ya kupaua.
Katika hatua nyingine, Chalamila ametembelea na kukagua barabara za Masaki wilaya ya Kinondoni na kukemea matumizi holela ya maeneo ya hifadhi ya barabara.
Pia uwekaji holela wa mabango ya matangazo barabarani, matumizi holela ya maeneo ya wazi, na ufanyaji holela wa biashara ambapo amesema Masaki ni eneo “Prime” kila kinachofanyika ni vema kuzingatia vigezo ambavyo ni rafiki.