Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Agosti 15, 2024 ametembelea na kufanya ukaguzi wa mwenendo wa utoaji huduma katika kivuko cha Feri – Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila wakati akikagua mwenendo wa utendaji kazi na mazingira ya kivuko hicho ameitaka TAMESA kufanya maboresho makubwa ya mazingira ya utoaji huduma ambayo yatakuwa rafiki kwa watu wote wanaotumia huduma hiyo ya kivuko.
Aidha RC Chalamila amesema ni vizuri kufungua milango kwa sekta binafsi kuwekeza katika kivuko hicho ili kuwe na huduma bora ambazo zitavutia wananchi mfano mzuri kwa sasa Kivuko binafsi kimekuwa kimbilio la watu kuliko kivuko cha Serikali tafsiri yake ni kuwa sekta binafsi inaweza kufanya vizuri zaidi.
” Rais hawezi kuwaamulia kila kitu ukipewa dhamana umeaminiwa , hivyo kuwa mbunifu”,amesema Chalamila.