Na Lucy Ngowi
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT), imefungia Majukwaa na Programu Tumizi 69, zilizokuwa zinajihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali kwa kutokuwa na leseni na idhini ya kufanya biashara hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba imeeleza kuwa majukwaa na programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu Agosti 27, 2024.
Tutuba amesema mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda mlaji wa huduma za fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.
Ametaja Majukwaa na Programu Tumizi hizo kuwa ni BoBa Cash, Hewa Mkopo, Money Tap, Soko loan, Bolla Kash – Bolla Kash Financial Credit, Hi Cash, Mpaso chap loan – Mkopo kisasa, Sunloan, BongoPesa-Personal Online Loan na HiPesa.
Mengine ni Mum loan, Sunny Loan,Cash Mkopo, Jokate Foundation Imarisha Maisha, My credit, Swift Fund, Cash pesa, KOPAHAPA, Nikopeshe App na TALA.
Pia Cash poa, Kwanza loan, Nufaika Loans, TikCash, CashMama, L-Pesa Microfinance, Okoa Maisha – Mkopofast, Twiga Loan, CashX, Land cash, Pesa M, TZcash, Credit Land, Loanplus, Pesa Rahisi, Umoja, Eaglecash TZ, M-Safi, PesaPlus, Usalama Na Uwakika Mkopo Dk15 na Fast Mkopo.
Vile vile Mkopo Express, PesaX, Ustawi loan, Flower loan, Mkopo Extra, Pocket loan, Viva Mikopo Limited, FUN LOAN, Mkopo haraka, Pop Pesa, VunaPesa, Fundflex, MkopoFasta, Premier loan, Yes Pesa, Get cash, MkopoHaraka, Safe pesa, ZimaCash na Getloan.
Nyingine ni Mkopohuru, SasaMkopo, Getpesa Tanzania, Mkoponafuu, Silk loan, Hakika loan, Mkopowako na Silkda Credit.
“Benki Kuu inautahadharisha Umma kutojihusisha na Majukwaa na Progamu Tumizi hizo ‘’Applications’. Aidha, Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia programu hizi ili kuepusha Umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali vya Mamlaka husika.
“Benki Kuu imechapisha na itaendelea kuhuisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma za mikopo katika tovuti yake,” imesema taarifa hiyo.