Na Mwandishi Wetu
MTIA nia wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani Bonifas Jacob amesema akishinda nafasi hiyo hatakaa ofisini.
Jacob maarufu kama ‘ Bonny Yai’ amesema hayo wakati akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Maelezo ya Jacob, baada ya kurudisha fomu hiyo,”Nitapiga ziara za Mkoa kwa Mkoa, Wilaya kwa Wilaya, Jimbo kwa Jimbo, Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa, Kitongoji kwa Kitongoji. Mwenyekiti wa Kanda atakuwa mtaani, hatakuwa ofisini,” .
Kwa upande mwingine, Jacob amesema endapo hatashinda nafasi hiyo hatalialia.
“Kama Kura hazitatosha hata nikishindwa sitapiga kelele ovyo kwa sababu nimeikosa nafasi hii. Nitachukulia wakati wangu bado,” amesema.