Na Mwandishi Wetu
KIGOMA: BARAZA la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Aidha baraza hilo na menejimenti limechangia Sh. Milioni moja kwa ajili ya Samia kuchukua fomu ya kugombea Urais,

Na Sh. 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Vuma Olle kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika Kikao cha Robo Mwaka, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Eliya Kagoma amesema
ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa ya maendeleo wilayani humo.
–

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmsahuri hiyo, Dkt.Semistatus Mashimba akizungumza kwa niaba ya watendaji wa Halmashauri, amesema wanaungana na Baraza hilo katika kumpongeza Rais Samia kwa fedha nyingi alizozipeleka kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayowanufaosha wananchi.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kasulu, Jennifer Chinguile amepokea mchango huo kwa niaba ya chama na kuahidi kuuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM,Balozi Emmanuel Nchimbi kabla ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwezi huu.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Simon Nzibuje ametoa shukrani kwa mchango huo na kuhaidi kuufikisha kwa mhusika.

Akitoa salamu za serkali, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kuwa na taadhari na kuhakikisha wanatunza chakula kutokana na hali isiyoridhisha ya usalama wa chakula kwa sasa.
