Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM :NAIBU Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Dustan Kitundula amesema Serikali Imejidhatiti katika kuhakikisha asali Inayozalishwa nchini Inakidhi ubora wa Kimataifa, hali itakayosaidia kuongeza mchango wa sekta ndogo ya nyuki katika ukiaji wa uchumi wa nchi.
Ameyasema Hayo leo Mkoani Dar es Salaam wakati wa Hafla ya Uwekaji Saini Itifaki Ya Kuuza Asali Ya Tanzania Nchini China.
Amesema kwa sasa Mapato yatokanayo na asali na bidhaa za nyuki ni takribani dola milioni 77 kwa mwaka hivyo kusainiwa kwa Mkataba huo kutatoa fursa kwa watanzania kuongeza uzalishaji zaidi.
Kwa Upande Wake Waziri Wa Utawala na Mkuu Wa Forodha Kutoka Jamhuri ya Watu wa China Yu Jianhua, amesema Nchi hiyo Ina Idadi kubwa ya watu na kwa Mwaka Inahitaji Takribani Tani Milioni 32
Hivyo ni fursa kwa watanzania kuongeza uzalishaji Ili kukidhi matakwa ya Soko hilo .
Naye Kaizirege Kamara ambaye ni mmoja wa Wafugaji wa Nyuki amesisitiza wadau wa sekta hiyo kuongeza uzalishaji huku akiipongeza Serikali kwa kuendelea kuongeza uwekezaji na kusaidia kukuza uchumi wa Wananchi.