Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema Aprili mwakani 2025, yatatolewa matokeo ya awamu ya kwanza ya maoni mbalimbali yaliyotolewa na vijana.
Ridhiwani ameyasema hayo katika Mkutano na Mtandao wa Vijana Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika Mkoani Dar es Salaam.
Amesema maoni hayo ya vijana yanasaidia kuchambua mtazamo unaotakiwa kuwepo, hivyo Kama Waziri mwenye dhamaba ya vijana atayasimamia maoni yote yaliyotolewa, kwa kuhakikisha yanaingizwa kwenye Dira ya Taifa.

“Maoni hayapigwi nyundo yanasikilizwa na kufanyiwa kazi yale jamii inayoyataka,” amesema.
Miongoni mwa maoni yaliyotolewa na vijana ni kuhusu namna gani nchi inapaswa kuwa na utaratibu wa kuwaandaa vijana,pia dira hiyo iainishe walau asilimia ya vijana wanaotakiwa kuwa kwenye vyombo vya maamuzi.
Pia rasimu iliyopo haijaainisha programu maalum ya kuwajengea uwezo wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na uwakilishi wa wenye ulemavu.
