MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Afya Bora Yachochea Ustawi wa Wananchi Kigoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Afya Bora Yachochea Ustawi wa Wananchi Kigoma
Habari

Afya Bora Yachochea Ustawi wa Wananchi Kigoma

Author
By Author
Share
4 Min Read
 Pato la Mwananchi Laongezeka kwa Asilimia 45.4
Na Danson Kaijage
DODOMA: MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Saimon Sirro amesema  maboresho makubwa katika sekta ya afya yamechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa ustawi wa wananchi wa Kigoma, hali iliyosababisha kuongezeka kwa pato la mtu mmoja mmoja kwa asilimia 45.4.
Ongezeko hilo ni katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma, Sirro amesema kuwa pato la mwananchi wa Kigoma limepanda kutoka Sh. Mil. 1.4 mwaka 2020 hadi Sh. Milioni 2.1 mwaka 2024.
“Kipato cha wananchi wetu kimeongezeka kwa kiasi kikubwa, na sehemu kubwa ya mafanikio haya yanatokana na uboreshaji wa huduma za afya, upatikanaji wa dawa, na kuimarika kwa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma,” amesema.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, Mkoa wa Kigoma umepokea jumla ya Sh. Bilioni 50.9 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya.
Amesema kiasi hicho cha fedha kimeboresha upatikanaji wa huduma bora za afya katika maeneo ya mijini na vijijini.
“Miundombinu ya afya imeimarika kwa kiwango kikubwa. Hospitali za wilaya zimeongezeka kutoka tatu mwaka 2020 hadi nane mwaka 2025. Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 34 hadi 53, na zahanati zimeongezeka kutoka 236 hadi 283,” amesema.
Aidha, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi umeongezeka kutoka asilimia 86 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 92 mwaka 2025 hatua inayowezesha wananchi kupata matibabu kwa wakati na kuzuia athari za kiafya zinazoweza kuathiri shughuli zao za uzalishaji.
“Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya afya njema na uwezo wa uzalishaji wa mtu mmoja mmoja. Wananchi wetu sasa wanatumia muda mwingi katika kazi na si kwenye foleni za hospitali,” amesema.
Mbali na mafanikio ya sekta ya afya, Sirro amebainisha kuwa hali ya uchumi wa mkoa imeendelea kuimarika, ambapo pato halisi la Mkoa limeongezeka kutoka Sh. Trilioni 4.1 mwaka 2020 hadi Sh. Trilioni 5.6 mwaka 2024 sawa na ukuaji wa asilimia 38.6.
“Kwa ujumla, Mkoa wa Kigoma umepokea zaidi ya Sh.Trilioni 11.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kati ya mwaka 2020 hadi 2025. Fedha hizi zimewekezwa kwenye afya, elimu, miundombinu na sekta nyingine muhimu,” amesema.
Katika upande wa elimu, Sirro amesema kuwa fedha za utekelezaji wa mpango wa elimu bila ada zimeongezeka kutoka Sh. Bilioni 9.60 mwaka 2020 hadi Sh. Bilioni 14.67 mwaka 2025. Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 664 hadi 742.
Amesema mafanikio hayo yanaonesha kuwa uwekezaji kwenye afya si tu kwamba unaokoa maisha ya watu, bali pia ni kichocheo kikuu cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kielimu kwa wananchi wa Kigoma.
“Afya njema ya wananchi wetu ndiyo msingi wa mafanikio haya yote tunayoyaona. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuwekeza katika ustawi wa Watanzania, hususan katika maeneo ya pembezoni kama Kigoma,” amesema.

You Might Also Like

Matwebe Aipongeza Serikali Kushirikisha JUMIKITA  Kwenye Shughuli Za Kitaifa

Dkt. Tumbo Aitaka Jamii Kuelimishwa Namna Bora Ya Kuhifadhi Taka

BRAC Tanzania: Upo Umuhimu Sekta Binafsi, Serikali Kushirikiana

Wakulima wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

BUWSSA Yapewa Bilioni 28 Kutatua Tatizo La Maji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CCM Yasitisha Ratiba ya Uchaguzi wa Maoni
Next Article Tumeleta Utulivu na Huduma kwa Walimu’ – Ikomba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Rais Mpya CWT Ikomba: ‘Nataka Kuwaunganisha Walimu, Kuitendea Haki Kazi Yetu’
Habari July 20, 2025
Tumeleta Utulivu na Huduma kwa Walimu’ – Ikomba
Habari July 20, 2025
CCM Yasitisha Ratiba ya Uchaguzi wa Maoni
Habari July 19, 2025
Uvuvi Wa Kisasa Wainua Mwanza Kiuchumi
Habari July 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?