Na Mwandishi Wetu
Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) amesema atavunja Bodi ya Korosho na bodi zote ili kuunda mamlaka moja ya mazao ya kimkakati.
Mwalim amesema serikali ya CHAUMMA itawaruhusu wakulima kuuza mazao yao popote wanapotaka ili wafaidi zao lao la biashara.
“Uzeni popote mnapotaka, iwe ndani au nje ya nchi, iwe China, kwa kuwa mimi siamini katika uuzaji wa stakabadhi ghalani.”
“Tuachane na ushamba huo wa stakabadhi ghalani… yanayotokea katika korosho na mbaazi ndiyo matokeo ya CCM.”
“Korosho usipoila kama tiba, utaila kama kiburudisho… korosho si ya mtu maskini ila nawashangaa wenye korosho yao maskini,” amesema na kuongeza, korosho ni zao pekee linalouzwa kwa mnada, tena mnada wa kwanza na wa pili.
Amewataka wananchi hao wasiuze korosho yao mpaka aapishwe Novemba mwaka huu ili aweze kuipandisha bei.
Kuhusu barabara, Mwalim amesema CCM imeshindwa kujenga sasa miaka 64 imepita.
“Wananchi wakilalamikia utasikia tupo kwenye upembuzi yakinifu… habari ndiyo hizo hizo.”
“Twendeni tukamchague rais kijana, nchi zenye marais vijana wana maendeleo.”