MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Balozi Sirro: Bila Amani, Maendeleo Hayapo Kigoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Balozi Sirro: Bila Amani, Maendeleo Hayapo Kigoma
Habari

Balozi Sirro: Bila Amani, Maendeleo Hayapo Kigoma

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

KIGOMA – KASULU: MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro amesema jiografia ya mkoa huo unaopakana na nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inaufanya kuwa eneo nyeti linalohitaji kudumisha amani kwa kila hali.

Sirro amesema hayo katika Kongamano la Amani la Kuliombea Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu (TCC).

Amesisitiza kuwa amani si chaguo bali ni msingi wa maendeleo kwa wananchi wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

“Bila amani, hakuna biashara ya mipakani, kilimo hakiwezi kustawi, uvuvi na biashara ndogondogo haviwezi kuendelea. Amani ni uti wa mgongo wa maendeleo,” amesema.

Pia amewataka viongozi wa dini kuepuka kuchanganya dini na siasa kwa kutumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa, kwa kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha mshikamano wa kijamii.
Habari Picha 9311

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu, amewapongeza viongozi wa dini kwa ushirikiano wao na serikali katika matukio mbalimbali, na kuwataka waendelee kuwaombea viongozi ili waweze kutoa maamuzi yenye busara kwa manufaa ya wananchi.

Habari Picha 9313

Naye Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Nasib Mungelwa, amesema kongamano hilo limeonesha mshikamano wa wananchi licha ya tofauti zao za kiitikadi, na kwamba hali hiyo inasaidia kuimarisha amani na umoja miongoni mwao.

Habari Picha 9314

Akichangia katika kongamano hilo, Askofu wa Kanisa la FPCT Jimbo la Kasulu, Shadrack Bunono, amesema viongozi wa umma wanapaswa kutumia busara na hekima katika maamuzi yao kwa manufaa ya wananchi. Aliongeza kuwa sala na maombi kwa viongozi ni msingi muhimu wa mafanikio ya wilaya hiyo.

Habari Picha 9308

Kongamano hilo limeandaliwa na Kamati ya Maridhiano kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, likilenga kuhimiza mshikamano, amani na maombi kwa ajili ya ustawi wa taifa.

You Might Also Like

Aprili 2025 Matokeo Awamu Ya Kwanza, Maoni Dira Ya Taifa Na Maendeleo 2050 Kutolewa

Mwenda: Tupo kwa ajili ya kuzitatua changamoto za wananchi

Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia kuhitimishwa DSM

CHAUMMA kuanzisha mjadala wa elimu ndani ya siku 100

Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ndizi, Mchele, Mafuta Vyapanda Bei
Next Article Mgombea Urais SAU Aahidi Kuongoza Nchi Kwa Hofu Ya Mungu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni
Habari October 28, 2025
Elimu Ya Nishati Safi Ya Kupikia Yawafikia Maofisa Dawati Ngazi Ya Mikoa Na Halmashauri
Habari October 27, 2025
Wananchi wahamasishwa kuandika historia mpya kupitia kura
Habari October 25, 2025
Shibuda: WanaMaswa jitokezeni kupiga kura bila woga
Habari October 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?