Na Lucy Lyatuu
TUME ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua kwa awamu ya pili ya udahili Kwa mwaka 2025/2026bao umeanza Leo Septemba 3 hadi Septemba 21 mwaka 2025.
Tume hiyo inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa hiyo kutuma maombi kwa vyuo wanavyovipenda.
Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya kukamilika kwa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Amesema waaombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa awamu ya pili kama ilivyo kwenye kalenda ya udahili katika tovuti ya TCU.
Profesa Kihampa amesema Tume inaelekeza vyuo vya elimu ya juu nchini kutangaza program ambazo bado zina nafasi nakutoa wito kwa waombaji wa udahili wa shahada ya kwanza kuwa masuala ya yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
Amesema kwa wale ambao watapata changamoto katika kujitihibitisha vyuo vyote vinaelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.
Ameeleza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza ya udahili wa shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika na majina ya waliodahiliwa katika awamu hiyo yatangangazwa na vyuo husika.
Ameongeza katika awamu ya kwanza jumla ya waombaji 146,879 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 88 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika shahada ya kwanza na jumla ya program 894 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na program 856 mwaka 2024/2026 ikiwa ni ongezeko la program 38 za masomo.
Vilevile kwa upande wa nafasi za udahili mwaka huu kuna jumla ya nafasi 205.652 ikilinganishwa na nafasi 3.3 katika program za shahada ya kwanza.
Amesema katika awamu ya kwanza jumla ya waombaji 116,596 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji wote waliiomba udahili wamepata udahili kweye vyuo walivyoomba ambapo idadi ya waombaji na watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika awamu ya pili ya udahili.
Hatahivyo amesema waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanafikia 67,576 ambapo wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja wapo kuanzia Leo(Sept 3,2025) hadi Septemba 21 mwaka huu,ambapo uthibitisho huo unafanyika kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au kwa barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.