MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali
Habari

Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali

Author
By Author
Share
5 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: SERIKALI kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeelezaTanzania inatarajia kuwa na muongozo mmoja wa kitaifa wa usimamizi wa takwimu kidijitali ifikapo Januari 2026.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Mifumo na Huduma za Uzingatiaji wa Sheria, Miongozo na Viwango vya TEHAMA,  wizarani hapo Mohamed Mashaka amesema tayari mazingira yameanza kuandaliwa kwa kupitia upya sera ya TEHAMA pamoja na miongozo mingine muhimu.
Habari Picha 9190
“Tunataka nchi iwe na muongozo mmoja wa kitaifa utakaosimamia matumizi ya takwimu kwa maendeleo. Takwimu ni nyenzo muhimu katika kukuza ubunifu na uchumi, na tunatarajia kuwa na mfumo wa usimamizi wa taarifa za kiserikali kwa njia ya kidijitali,” amesema Mashaka.
Ameongeza lengo ni kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa takwimu utakaosaidia kupanga, kutunza na kutumia taarifa hizo katika sekta mbalimbali kama kilimo, afya, hali ya hewa na maendeleo ya kijamii.
Mashaka ameeleza kuwa changamoto kubwa kwa nchi nyingi za Afrika ni ukosefu wa miundombinu ya kuhifadhi takwimu, hali inayosababisha taarifa nyingi kuhifadhiwa nje ya nchi.
Amesisitiza kuwa Tanzania inahitaji kuwa na miundombinu imara ili kuhakikisha taarifa zote zinabaki ndani ya nchi.
Habari Picha 9193
“Kwa sasa tuna vituo vinne vya serikali vya kuhifadhi taarifa. Hii haitoshi. Tunahitaji miundombinu ya kutosha ili tufanikishe azma ya kujenga uchumi wa kidijitali,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu katika wizara hiyo, Leo Magomba, amesema jukumu lao ni kuwezesha uchumi wa kidijitali kupitia miundombinu bora ya TEHAMA.
“Miundombinu ni msingi wa kila kitu. Ili taarifa zisafirishwe, kuchakatwa na kuhifadhiwa inahitajika miundombinu ya uhakika,” amesema Magomba.
Ameeleza hadi sasa wilaya 109 kati ya 139 nchini zimeunganishwa na mkongo wa taifa wa mawasiliano, na watu zaidi ya 14,000 wameunganishwa.
Habari Picha 9197
Aidha, Tanzania imeunganisha mkongo wake na nchi jirani kama Kenya (kupitia Horohoro, Namanga na Sirari), Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Msumbiji.
Mipango inaendelea kuiunganisha pia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ifikapo Septemba 2025.
“Tanzania pia imeunganishwa na mataifa mengine kupitia mikongo ya baharini, ikiwa ni pamoja na visiwa vya Shelisheli. Tuna vituo sita vya kimataifa vya kubadilishana taarifa vilivyopo Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Zanzibar,” amesema.
Serikali pia inaendelea na mradi wa kuhakikisha shule zote zinapata huduma ya intaneti ifikapo mwaka 2030. Aidha, imeongeza juhudi kuhakikisha watumishi wa umma na wananchi wanatumia huduma za intaneti katika maisha ya kila siku.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Dkt. Emmanuel Mkilia amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana kulinda faragha za watu, Tanzania tayari imetunga sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na pia imeweka kanuni za utekelezaji wake.
“Mkutano huu ni sehemu ya kujenga uelewa kwa wadau kuhusu umuhimu wa kulinda taarifa binafsi kwa kuwa faragha ni haki ya msingi ya binadamu,” amesema Dkt. Mkilia.
Amesema sheria hiyo inasaidia kujenga uaminifu kwa watumiaji wa mifumo ya kidijitali, jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wa kidijitali. Aliongeza kuwa matumizi ya mifumo iliyounganishwa  yanaongeza changamoto ya kulinda faragha, hivyo sheria hiyo inaleta mazingira bora ya kiusalama.
Habari Picha 9191
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Soft Tech Consultants Ltd, Parish Bhatt, amesema kuwa usimamizi wa takwimu unapaswa kuzingatia matumizi salama na yenye tija ya taarifa hizo, hasa wakati huu ambapo akili mnemba inahitaji takwimu bora ili kufanya kazi kwa ufanisi.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Haruni Matagane, amesema kabla ya mwaka 2022, hakukuwa na sheria mahsusi ya kulinda taarifa binafsi. Badala yake, kulikuwepo na sheria ya uhalifu wa kimtandao.
“Hata hivyo, baada ya mwaka 2022, tulitunga sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ambayo imeeleza makatazo mbalimbali kuhusu namna taarifa za watu zinavyopaswa kushughulikiwa,” amesema Matagane.
Amesema sheria hiyo pia inaruhusu taarifa kutoka nje ya nchi kwa masharti maalum, na sasa serikali iko katika mchakato wa kutunga sheria mahsusi ya kusimamia masuala yote ya TEHAMA ili kuimarisha usalama, maendeleo na ufanisi wa matumizi ya teknolojia nchini.

You Might Also Like

Rais Samia Awakumbuka Wazazi Wanaojifungua Watoto Njiti

Mfumo Uendeshaji Mashauri Kidigitali Kwa Watumishi wa Umma Uharakishwe

VETA yawafikia madereva ‘Boda boda’

Utafiti Wa Roketi UDOM Uko Mbioni Kukamilika

Waziri Mkuu Aagiza Kuimarisha Ufuatiliaji Na Tathmini Kuleta Maendeleo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vitongoji 1997  Vimepatiwa Huduma Ya Umeme, Kilimanjaro  
Next Article CCCC Yagusa Wanafunzi Msasani kwa Msaada wa Vifaa vya Shule, Chakula
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?