MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yaibuka Kidedea Maonesho Zambia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yaibuka Kidedea Maonesho Zambia
Habari

Tanzania Yaibuka Kidedea Maonesho Zambia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
LUSAKA – ZAMBIA: TANZANIA imeibuka mshindi wa pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki Maonesho ya 97 ya Kimataifa ya Kilimo na Biashara yaliyofanyika Lusaka, Zambia, kuanzia Julai 29 hadi Agosti nne,  mwaka huu 2025, Zimbabwe ikishika nafasi ya kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti nane, 2025 katika ukumbi wa MOI, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema ushindi huo umetokana na elimu na maelezo ya kitaalamu kuhusu huduma za afya za kibingwa na kibobezi kutoka Tanzania, pamoja na mchango wa sekta ya usafirishaji.
“Taasisi tano kutoka Tanzania zilishiriki, zikiwemo MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), na Shirika la Ndege la ATCL. Kwa pamoja tumefanya vizuri na kushika nafasi ya pili,” amesema.
Amesema ushiriki wa taasisi za afya ulilenga kuhamasisha utalii wa tiba, kwa lengo la kuwavutia wagonjwa kutoka Zambia kuja kupata huduma bora za afya Tanzania badala ya kwenda nje ya bara la Afrika ambako gharama ni kubwa.
“MOI na JKCI tunatoa zaidi ya asilimia 96 ya matibabu ya magonjwa ya moyo, mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu. Tukiwa Zambia, taasisi hizi tatu za afya ziliweza kuhudumia watu 911, kati yao 105 wameahidi kuja Tanzania kwa matibabu zaidi,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tiba Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, amesema kamati hiyo imewekeza nguvu kubwa katika kujitangaza ili kuwavutia wagonjwa kutoka mataifa mengine kuja kutibiwa Tanzania.
“Awali tulikwenda visiwa vya Comoro na kutoa huduma kwa watu 2,292. Hadi sasa tumepokea wagonjwa zaidi ya 150 waliokuja kutibiwa katika hospitali zetu za MOI, MNH, JKCI na Ocean Road. Haya ni matunda ya ushiriki wetu kwenye maonesho kama haya,” amesema Dkt. Kisenge.
Amesema kuja kwa wagonjwa kutoka nje kunachangia ukuaji wa uchumi wa taifa:, “Watakuja kulala katika hoteli, kununua chakula na kupata huduma mbalimbali,  haya yote yanaongeza pato la taifa. Ndiyo maana tunaita tiba utalii  mtu anatembelea nchi yetu kwa ajili ya kupata matibabu.”
Ushiriki wa Tanzania uliratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia chini ya Balozi Mathew Mkingule. Banda la Tanzania lilitembelewa pia na Rais wa Zambia, Hakainde Hichelema, Agosti mbili, 2025.

You Might Also Like

Kifo cha Ndugai Kisigeuzwe Siasa – Familia

TSB, Wizara ya kilimo yaweka mpango wa vituo vya usindikaji mkonge

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa Suluhu Sports Academy

Wiki ya Huduma za Fedha: SELF Yafungua Fursa za Kiuchumi kwa Wananchi Tanga

Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article MSD, SALAMA Zaunganisha Nguvu Kuboresha Sekta ya Afya SADC
Next Article Tari Ilonga yaboresha mbegu, mavuno yapanda hadi tani 3.8 kwa hekta
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TMA Yakamilisha Ufungaji Mitambo Ya Uangalizi Mpanda, Pemba
Habari May 13, 2026
Abiria Mil 2.51  Wasafirishwa Na SGR Kuanzia Julai 2025 Hadi Sasa
Habari May 13, 2026
Shehena  Inayohudumiwa Bandarini Yaongezeka  Kufikia Tani Mil 27.76
Habari May 13, 2026
TARURA Wataka Makandarasi Kulinda Njia Mbadala Kipindi cha Mvua Kubwa
Habari May 10, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?