Na Danson Kaijage
DODOMA: SPIKA wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, ametangaza kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Ndugai pia alikuwa ameshiriki kwenye kura za maoni kutetea nafasi yake ya ubunge katika Jimbo la Kongwa, jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Dkt. Tulia kupitia Kitengo cha Mawasiliano cha Bunge, imeelezwa kuwa leo Agosti sita, 2025 , Job Ndugai amefariki dunia.
Hata hivyo, taarifa hiyo haijafafanua chanzo cha kifo chake wala muda halisi wa kufariki, na badala yake imeelezwa kuwa Kamati ya Mazishi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu taratibu za mazishi.
Taarifa ya Spika Dkt. Tulia imetoa pole kwa wakazi wa Jimbo la Kongwa, Mkoa wa Dodoma, familia na Watanzania kwa ujumla.