MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Wajitosa Kugombea Ubunge
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Wajitosa Kugombea Ubunge
Habari

Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Wajitosa Kugombea Ubunge

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi

VIONGOZI mbalimbali kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wamejitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge kupitia majimbo na viti maalum, kutokana na uteuzi wa awali wa wagombea nchini.

Katika Mkoa wa Mtwara, Asha Moto, ambaye ni Katibu wa Wanawake wa TUCTA, anawania Viti Maalum.

Asha amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki za wanawake mahali pa kazi na kupigania mazingira bora ya kazi, anachuana na Agnes Hokororo, Dkt. Rahman Hingora, Athumin Mapalilo, Days Ibrahimu na Jane Chikomo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) , Joel Kaminyoge, amepitishwa kuwania Jimbo la Ileje.

Klaminyoge anachuana na wagombea wengine akiwemo Stella Fiyao, Godfrey Msongwe, Eliud Ndabila, Epson Ngambo, Ezekiel Kibona na Claudio Kitta.

Miongoni mwa viongozi wengine waliojitokeza ni Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Ronward Mwashiuya, anayewania Jimbo la Songwe.

Wagombea wengine katika jimbo hilo ni Philipo Mulugu, Philemon Msomba, Maria Bilia na Tedius Mwachipindi.

Pia Katibu Mkuu wa TALGWU, Rashid Mtima, yupo kwenye kinyang’anyiro cha Jimbo la Newala Mjini, akichuana na Zafarani Madayi, Zuhura Mkumba na Yahya Mnung’a.

Kwa upande wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Utafiti, Taaluma na Mashirika (RAAWU), Jane Mihanje, anawania nafasi hiyo sambamba na Amina Karuma, Sheila Lukuba, Hajira Mwikoko, Lucy Kombani, Kulwa Kangeta, Aliyah Omar, Rachel Mashishanga na Josephine Kupuna.

Mkoani Katavi, Katibu wa TALGWU mkoa huo, Angela Ntemo, anagombea nafasi ya Viti Maalum akiwa pamoja na Martha Mariki, Askari Mbogo, Fortunately Kabeja, Stella Chenchele, Janeth Pinda, Elizabeth Sultan na Mahija Nyembo.

Aidha, Silfa Kapinga, Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka TUICO, ameomba kuteuliwa kuwania Viti Maalum vya wafanyakazi.

TUCTA ni shirikisho linalounganisha vyama mbalimbali vya wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi nchini, likishughulikia masuala ya ustawi wa wafanyakazi, haki zao, usalama kazini, na kutoa sauti ya pamoja katika majadiliano na serikali au waajiri.

Vyama vilivyo chini ya TUCTA ni pamoja na: Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu (RAAWU), Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Chama cha Wafanyakazi wa Migodini, Nishati na Ujenzi (RAMICO), Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano (COWTU( T) na vinginevyo.

You Might Also Like

Dkt Yonaz Awaasa Watumishi Ofisi Ya Waziri Mkuu  Kuongeza Bidii Katika Kutekeleza Majukumu Yao

WCF Yatakiwa Kuongeza Nguvu Kusajili Waajiri

UDSM  Yakamilisha Utafiti Wa Dawa Ya Kusafisha Sumu Kwenye Maji

Hazina yaanza kuwalipa wanachama 465 wa TALGWU

Rais Mwinyi adhamiria kusimamia ubora wa bidhaa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wafanyakazi Majumbani Walia: ‘Tunaishi Katika Mazingira Hatarishi’
Next Article Rais CWT Ni Kiongozi Aliyekuza Taaluma Kwa Moyo, Sio Cheo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wakazi Wa Ntyuka Wataka Kiongozi Mchapakazi
Habari August 1, 2025
Kisaro Ahojiwa Kuhusu Migogoro ya Ardhi,  Mwinje Ajitosa na Suluhisho la Miundombinu na Umiliki wa Ardhi
Habari August 1, 2025
Rais Samia Aipa Neema Miradi Ya Kuzalisha Umeme Iringa
Habari August 1, 2025
Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini
Habari July 31, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?