MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu
Habari

Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
KIBAHA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameipongeza Shule ya Sekondari Kibaha kwa kuwa miongoni mwa shule bora nchini kwa matokeo ya mitihani ya kitaifa, huku akitoa wito kwa walimu na uongozi wa shule hiyo kuhakikisha kiwango cha ufaulu hakishuki.
Mchengerwa ametoa pongezuli hizo akiwa kwenye ziara, ambapo alikagua miundombinu ya shule hiyo ikiwemo madarasa, mabweni, maabara, na maeneo ya wanafunzi wa bweni, kabla ya kuzungumza na walimu pamoja na wanafunzi waliokuwa wakijiandaa kuanza kidato cha tano.
“Nawapongeza sana kwa matokeo mazuri ambayo yanaifanya Kibaha kuwa alama ya ubora wa elimu nchini. Hata hivyo, changamoto ya sasa ni kuhakikisha mnaendelea kushikilia kiwango hiki au kupanda zaidi licha ya ongezeko la wanafunzi,” amesema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Pwani,  Jimmy  Nkwamu amesema ufaulu wa mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu umefikia asilimia 93.7, ambapo wanafunzi 136 kati ya 140 walipata daraja la kwanza.
Aidha, kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024, asilimia 52 ya wanafunzi walipata daraja la kwanza, huku hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la tatu, la nne, au la sifuri.
Mchengerwa ameridhishwa na juhudi za walimu na uongozi wa shule hiyo, akisisitiza kuwa Kibaha Sekondari ni mfano wa kuigwa katika sekta ya elimu.
Amesema ni muhimu kwa shule hiyo kuwa na mikakati madhubuti ya kitaaluma na kitaasisi ili kuhakikisha kuwa ubora unaendelea kuimarika licha ya changamoto ya ongezeko la wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu.
“Nataka kuona mikakati ya kudhibiti changamoto zitokanazo na idadi kubwa ya wanafunzi. Walimu mnatakiwa kuwa wabunifu zaidi ili kutobadili mwelekeo huu mzuri,” amesema.
Kwa upande mwingine Waziri Mchengerwa  ametoa agizo kwa Ofisa Elimu wa Mkoa kufanya ziara katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani ili kubaini changamoto za kielimu na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
“Nakuagiza ufanye ziara katika kila wilaya ya mkoa huu na kuhakikisha changamoto zote za kielimu zinaainishwa na kutafutiwa suluhisho. Hatutaki kuona maeneo ambayo yanazorota kimatokeo wakati wengine wanapaa,” amesema.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu kwa kuhakikisha uboreshaji wa miundombinu, mazingira ya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji wa elimu katika ngazi zote.

You Might Also Like

Ridhiwani Apongeza Kurudi Kwa Gazeti La Mfanyakazi TANZANIA

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

Masauni Akabidhi Polisi Magari 77

RAAWU na mafanikio iliyopata utawala wa Rais Samia

Makala: Hakuna Kupita Bila Kupingwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani
Habari July 9, 2025
Katiba Na Sheria Kutoa Kipaumbele Kusikiliza Malalamiko Ya Wananchi
Habari July 9, 2025
Vumbi la Nyuki Lapewa Uzito Singida: Latajwa Tiba ya Asili Yenye Virutubisho 99
Habari July 9, 2025
Sirro: Kasulu Itambue Thamani ya Uwekezaji, Itenge Maeneo Rasmi
Habari July 9, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?