Na Lucy Lyatuu
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imebuni bajaji inayotumia maji na mafuta lengo likiwa ni kupunguza gharama za uendeshaji kwani injini inapopoa hutumia mafuta kidogo.
lMbunifu Andrew Mbanga kutoka ndaki ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) Ya Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) ameeleza hayo katika Banda la UDSM lililoki katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimaraifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema uwepo wa mfumo wa maji katika bajaji ni moja ya njia inayoweza kupunguza gharama za uendeshaji kwani injini inapopoa hutumia mafuta kidogo
Amesema ubunifu huo unatokana na biashara ya usafirishaji inavyozidi kukua nchini, ambapo watu wanaendelea kubuni namna rahisi ambazo zitawawezesha watu kufanya shughuli zao kwa urahisi.
Amesema Hiyo unatokana na kuwatafutia suluhisho linaloweza kuwapunguzia gharama za uendeshaji.
Amesema kwa mara ya kwanza alitengeneza bajaji ya aina hiyo mwenyewe lakini alipoambiwa kupeleka chuo Kikuu cha Dar es Salaam ifanyiwe marekebisho ilibainika kuwa imekaa muda mredu baada ya kufanyiwa vipimo.
Amesema ilibidi kuanza upya kwa kwa kushirikiana na wahandisi wa chuoni hapo, hadi walipoikamilisha na kuwa kama inavyoonekana kwa sasa.
Kuhusu inavyofanya kazi, Mmbaga amesema bajaji hiyo ina mfumo wa kuingiza maji kwa ajili ya kupooza ‘cylinder’ zisipate moto ambapo maji huwekwa katika tanki maalumu.
Amesema Maji hayo huenda kwenye injini yakiwa ya moto na kuingia katika rejeta na kwa kuwa Kuna feni katika rejeta hufanya maji yapoe na kuanza mzunguko mpya.
“Hilo linafanya injini inapoa muda mwingi hali inayofanya mafuta kidogo kutumima ukilinganisha na mfumo huo ungekosena,” amesema.
Amesema maji yanayotumika ni safi isipokuwa yasiyokuwa ya chumvi na hufanya kazi kwa wiki moja na mtu anatakiwa kubadilisha ikiwa mtu anafanya kazi kila siku.
“Ukiacha yachafuke sana yataziba matundu ya rejeta kwa sababu maji yanapozidi kuwa ya moto sana yanatengeneza povu, sasa povu likiendelea kukaa ndani ya rejeta na ikiwa ni maji ya chumvi ndiyo kabisa yanaziba matundu,” amesema.
Amesema bajaji za abiria za kawaida hazina mfumo wa maji isipokuwa zile za mizigo huku akisema lengo ni kufungua kiwanda cha kutengeneza bajaji.
Amesema watatengeneza bajaji aina tatu, ya kutumia gesi, bajaji za umeme jua na bajaji za kutumia mafuta ya kawaida,” amesema Mbanga.
Amesema wanatazamia kufanya biashara na watu wa ndani na nchi za jirani na sasa anaikiri tayari kupata oda za watu wanaotaka kutengenezewa bajaji hizo.
“Tukimaliza sabasaba tutakwenda Costecj ili bajaji iweze kuthamini na baadaye itaingia katika majaribio rasmi barabarani, baada ya uthamini tutaweza kupanga bei ambayo mteja anaweza kulipia,” amesema.