Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MWANAFUNZI wa Mwaka wa Pili, Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mtwara, Jeremia Mirobo amebuni mfumo wa usalama majumbani.
Mirobo ambaye amesomea fani ya umeme wa majumbani amebuni mfumo wa kuzima taa au umeme ambao unamzuia mtu asisogele luninga kwa sababu ya usalama wa macho yake.
Pia mfumo huo ukiwa umefungwa, kisha gesi ikawa inavuja ndani ya nyumba, huo mfumo utazima umeme kisha, utarudisha umeme gesi itakapoisha.
“Kuna wale ambao hawana mikono hivyo hawawezi kuwasha taa kwa kubonyesha, kwa hiyo watapuliza kuwasha, watapuliza tena kuzima,” amesema.
Ameongeza kuwa mfumo huo alioufanyia utafiti mtu anaweza kuuendesha akiwa mbali, na kutolea mfano mtu akiacha taa zinawaka kwa kusahau kuzima, kwa kutumia simu ya mkononi iliyounganishwa za mfumo itawezekana kuizima popote mtu huyo atakapokuwa.