MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Sanaa, Utamaduni Yaimarisha Urafiki Wa China, Afrika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Sanaa, Utamaduni Yaimarisha Urafiki Wa China, Afrika
Makala

Sanaa, Utamaduni Yaimarisha Urafiki Wa China, Afrika

Author
By Author
Share
6 Min Read

Na Waandishi Wetu

MAONESHO ya Mawasiliano ya Utamaduni ya China na Afrika, yenye kauli mbiu isemayo ‘ Harufu ya Pamoja, Kutembea Katika Njia ya Kisanaa Pamoja,’ yalifanyika hivi karibuni mjini Shanghai.

 

Lengo la Maonesho hayo ilikuwa ni kuanzishwa kwa Kituo cha Sino-Afrika mjini Shanghai,

 

Pia lengo lingine ni kukuza mawasiliano ya kitamaduni na kirafiki kati ya China na Afrika kupitia utamaduni na sanaa.

 

Maonyesho hayo yaliandaliwa na wadau mbalimbali wakiwemo, Kituo cha Mafunzo ya Michezo na Sanaa kwa Walemavu wa China, Kituo cha Noble cha Shanghai,

 

vile vile Kituo cha Mabadilishano ya Utamaduni ya Sino-Afrika (Shanghai), Kituo cha Mabadilishano ya China na Zimbabwe, na Mtandao wa Utafiti wa Uhusiano wa China-Africa wa Shanghai.

 

Maonyesho hayo  yalishirikisha kazi za kisanaa, uchezaji ngoma na mchakato wa mawasiliano.

 

Kwa kusudi la kutoa heshima kwa Siku ya Afrika kupitia sanaa, tukio hilo  lilionyesha uzuri na haiba ya kipekee ya utamaduni wa Kiafrika.

 

Katika tukio hilo, Watazamaji walikula chakula cha jadi cha Kiafrika na kuthamini muziki na picha za kuchora ambazo ziliunganisha tamaduni za Wachina na Waafrika.

 

Aidha, wasanii wa Kiafrika walichochea maadhimisho hayo kupitia kupiga ngoma za Kiafrika na kuimba wimbo wa Kishona Madiro.

 

Ingawa bendi maalumu inayoundwa na wanamuziki wa kijana wa Kichina hawakuweza kusoma alama za muziki kwa sababu ya ulemavu wa macho, wanamuziki hao walitumia midundo myepesi na hisia za dhati kuonyesha nguvu ya upendo na uvumilivu kupitia muziki.

 

Baadaye, wasanii wa China na Afrika waliimba wimbo ‘You Raise Me Up’ pamoja, ambalo lilimaanisha daraja la kuvuka mipaka ya kitamaduni na kitaifa na kuwaletea watazamaji karamu ya kisanaa.

 

Hali kadhalika, tukio hilo pia lilishuhudia ufunguzi rasmi wa Kituo cha Sino-Afrika (Shanghai), likiwa hatua muhimu katika mchakato wa ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Afrika.

 

Kituo cha Sino-Afrika (Shanghai) kinalenga kuwa jukwaa la maingiliano la pande mbili ili kukuza mazungumzo ya kitamaduni, ushirikiano wa kisanii na mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Afrika.

 

Licha ya kutoa huduma bora kwa wafanyakazi wa kujitolea wa China na taasisi nyingine zinazoshughulikia ushirikiano wa China na Afrika, kituo hiki kitatoa rasilimali nyingi na fursa muhimu katika nyanja mbalimbali kama vile utamaduni, elimu na biashara, ili kuwawezesha vijana, wasanii na wajasiriamali wa Afrika nchini China na kuwasaidia kupata maendeleo mazuri zaidi.

 

Siku hiyo Kituo cha Noble, Kituo cha Mabadilishano ya Utamaduni ya Sino-Afrika (Shanghai) na Kituo cha Sino-Afrika (Shanghai) vilitia saini katika Makubaliano ya Ushirikiano. Kwa ajili ya kutoa michango mikubwa kwa maendeleo ya maslahi ya umma.

 

Vituo hivi vitashirikiana katika maeneo mengi, kama vile kukuza maendeleo ya kiwango cha juu ya watu wenye ulemavu wa China, kuboresha hali ya maisha katika maeneo maskini ya Afrika, na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.

 

Miaka hivi karibuni, harakati za mawasiliano ya kitamaduni na kisanii kati ya China na Afrika zinaendelea motomoto.

 

Mnamo mwaka 2023, wimbo wa Kiswahili Malaika, ambao unabeba hisia za dhati za watu wa Afrika Mashariki, uliimbwa na kuonyesha haiba ya kitamaduni katika jukwaa la Michezo ya Gala ya Sikukuu ya Spring, ambalo linabeba kumbukumbu ya pamoja ya wachina bilioni 1.4. Mwaka 2024,

 

Tamasha la Nane la Vijana la China na Afrika lilifanyika kwa mafanikio, na wawakilishi wa vijiana zaidi ya 60 kutoka Afrika walitembelea mjini Beijing na Zhejiang nchini China.

 

Filamu na televisheni za Kichina, kama vile Minning Town na Doudou na Mama Wakwe Zake, zilitafsiriwa katika Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa, zilipokelewa vyema na watazamaji katika nchi nyingi za Afrika.

 

Mwaka 2025, “Viumbe wa Kiroho: Maonyesho ya Kisanaa ya Vinyago ya Kiafrika” yalifanyika kwa mfululizo katika makumbusho mkoani Henan, Shanxi na maeneo mengine nchini China.

 

Msingi na uhai wa uhusiano kati ya China na Afrika upo kwa watu, na maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika yatawahudumia watu zaidi.

 

Hivi sasa mawasiliano na ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Afrika umezaa matunda mengi, ambalo linaweka msingi imara wa umma kwa ajili ya kujenga pamoja Jumuiya ya Ngazi ya Juu ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.

 

Kutoka kwa sanaa hadi maono, kutoka kwa sauti hadi vitendo, mawasiliano ya kisanaa na kitamaduni kati ya China na Afrika yameonyesha wazi mshikamano wa tamaduni mbalimbali, uvumilivu na kujifunza, na ushirikiano wa kupata maslahi kwa pande mbili.

 

Pamoja na maendeleo makubwa ya miradi kama Kituo cha Sino-Afrika (Shanghai), mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Afrika yatakuwa na mustakabali wenye uhusiano wa karibu na ubunifu zaidi, huku yakiendelea kuwa kiwango kipya cha “safari ya kuelekeana’.

Mwandishi Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).

Barua pepe:02706@shisu.edu.cn

{

Mwandishi Song Yiting, mwanafunzi wa shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).

Barua pepe:Yiting_Mo@126.com

 

You Might Also Like

OSHA yaelimisha sheria mahala pa kazi kwa JOWUTA

Kitabu cha Utamaduni na Maendeleo Nchini Tanzania, Chaimarisha Mawasiliano ya Kitamaduni Baina ya China, Tanzania

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika

Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja

Tujenge Jumuiya Yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Afrika – Wang Yi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mchumi Ajitosa Kuwania Ubunge Manyoni
Next Article TTCL Yaweka Punguzo Kubwa Kwa Vifaa Vya Mobile Kwenye Sabasaba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TEA Yawaalika Wananchi Kujifunza SDF Unavyofanya Kazi
Habari July 3, 2025
Wanufaika wa SDF Waeleza Mafaniko Waliyoyapata
Habari July 3, 2025
VETA Dodoma Waleta Mashine Kurahisishia Upekechuaji Wa Alzeti
Habari July 3, 2025
VETA Shinyanga Waja Na Mafunzo Ya Saluni, Mapambo, Urembo
Habari July 3, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?