MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Madini Yaweka Rekodi Makusanyo Ya Maduhuli
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Madini Yaweka Rekodi Makusanyo Ya Maduhuli
Habari

Madini Yaweka Rekodi Makusanyo Ya Maduhuli

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: SEKTA  ya Madini imekusanya Maduhuli ya kiasi cha Sh. Trilioni moja ikiwa imebaki siku moja tu kukamilisha Mwaka wa Fedha 2024/25.
Katibu Mkuu wa  Wizara ya Madini, Yahya Samamba  amesema hayo wakati akifunga Bonanza lililowakutanisha pamoja watumishi wa Wizara na taasisi ambapo wameshiriki katika michezo mbalimbali.
Amesema katika Mwaka wa  Fedha 2024/25 Sekta ya Madini ilipangiwa kukusanya shilingi trilioni moja ambazo zimeingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
“Tumeweza kukusanya trilioni moja na ‘point’ bila kuwepo mgodi mpya, hakuna mwaka huko nyuma tuliosogelea  Sh. Bilioni 900  lakini mwaka huu tumeweza kukusanya kiasi hicho hii ikiwa ni sawa na wastani wa kukusanya Sh. Bilioni 84 kila mwezi,” amesema.
Amesema mwenendo mzuri wa ukusanyaji wa fedha umeifanya wizara kupangiwa kukusanya Sh. Trilioni 1.2 , hivyo, kuwataka watumishi kuongeza bidii ili Sekta ya madini iwe moja ya taasisi ambazo zitaongeza mapato ya ndani ya nchi yatakayoiwezesha nchi kujitegemea.
Kutokana na mafanikio hayo,  Samamba amewapongeza watumishi wote wa Wizara ya Madini na taasisi zake na kueleza kuwa, mafanikio hayo yametokana na mchango wa kila mtumishi kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
Amewataka  kuendeleza mshikamano na kufanya kazi kwa weledi ili Sekta ya Madini iendelee kutoa manufaa ya kiuchumi kwa Taifa.
Pia amepongeza Serikali kupitia Benki  Kuu ya Tanzania ( BoT)  kuanza kununua dhahabu kama akiba ya taifa na kusema suala hilo si dogo.
Amemwagiza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kuweka utaratibu wa kuwa na mabonanza yasiyopungua mannne Kwa mwaka kuendelea kujenga umoja na mshikamano baina ya watumishi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Tume ya Madini Dkt Janeth Lekashingo  amewataka watumishi kuendelea kujenga uhusiano na mawasiliano miongoni mwao huku akisititiza kujenga tabia ya kufanya mazoezi.

You Might Also Like

Mafunzo ya Ufundi Sasa Kupatikana Popote Kupitia Programu ya VSOMO”

Dar Sasa Kufanya Biashara Saa 24, Kuanza Februari 22 Mwaka Huu

Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

Biashara kidijitali inawezekana soko huru la Afrika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Washauri Serikali Kutumia Fedha Za Miradi
Next Article Wakili Kanyama Achukua Fomu Mtumba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64
Habari December 9, 2025
Profesa Ndunguru: Mtafiti Aliyejitoa Kusaidia Dunia Kupata Chakula Cha Baadae
Makala December 9, 2025
Profesa Ndunguru Abainisha Mwelekeo Mpya Wa Mageuzi Ya Kilimo Duniani
Habari December 9, 2025
TPDC na PURA Hakikisheni Watanzania Wananufaika na Rasilimali za Mafuta na Gesi- Salome
Habari December 8, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?