Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 4

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’

Na Mwandishi Wetu
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata elimu ya hifadhi ya jamii katika banda la NSSF wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili kwa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiri wenyewe,
Vile vile wananchi wanapewa elimu jinsi wanavyoweza kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja na elimu kuhusu huduma za kidijiti (NSSF Portal).
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.