MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Viongozi Bora Hujenga Mazingira Wezeshi Kwa Wahadhiri – Profesa Nombo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Viongozi Bora Hujenga Mazingira Wezeshi Kwa Wahadhiri – Profesa Nombo
Habari

Viongozi Bora Hujenga Mazingira Wezeshi Kwa Wahadhiri – Profesa Nombo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

PWANI: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema viongozi bora hujenga mazingira wezeshi kwa wahadhiri na watafiti kustawi , kupanda vyeo kwa haki bila mizengwe na kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa manufaa ya taifa.
Profesa Nombo amesema hayo alipokuwa akihitimisha Warsha ya Mafundo na Tafakuri kwa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), iliyofanyika Katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani,
Pia amewataka viongozi wa Vyuo Vikuu nchini kuendelea kuwa nguzo ya mabadiliko chanya kwa kukuza mazingira ya ubunifu, utafiti wenye tija na maendeleo ya kitaaluma yanayozingatia haki na uwazi.
“Uongozi wa vyuo vikuu unapaswa kuwa chachu ya ubunifu, utafiti wenye tija na machapisho ya kitaaluma yanayochangia maendeleo ya jamii,” amesema.
Amewapongeza viongozi wapya walioteuliwa na kuwatakia kila la heri katika majukumu waliyopewa
Pia kwa wale wanaoendelea na uongozi amewataka kuendeleza mafanikio waliyofikia na kuacha alama ya uongozi bora katika taasisi hiyo,
“Mungu awabariki muongoze vyema , awape hekima na uvumilivu katika utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema.
Naye Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye amesema kuandaa warsha kama hiyo kunahitaji rasilimali watu na fedha hivyo ametambua mchango wa wadhamini wote waliofanikisha shughuli hiyo.
Amesema elimu waliyoipata kwenye mafundo hayo iwe chachu ya kuendeleza misingi ya utawala bora, ubunifu na mwelekeo wa kimkakatikatika kuifikisha taasisi yao katika dira  yake ya mwaka 2061.
” Basi sote hatuna budi kuwa mabalozi wa mabadiliko chanya kwenye maeneoyetu ya kazi,” amesema.

You Might Also Like

Ridhiwani Aiagiza CMA Kushughulikia Migogoro Kwa Haraka, Ufanisi

Japan Yatoa Bilioni 27 Kuboresha Sekta Ya Afya

TARURA Yatenga Milioni 580 Kuboresha Barabara Zinazohudumia Sekta ya Madini Geita

VETA Mikumi Yatengeneza Mashine Ya Kuchakata Majani Ya Mifugo

Mwalim: Mchagueni Mwalimu Wangu Wa Siasa Shibuda

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Sheria Ya Kupata  Taarifa, Ya NGOs Zina Upungufu 
Next Article Wanafunzi 431, Watumishi 52 Watembelea TARI kujifunza Kilimo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?