Na Danson Kaijage.
WATANZANIA wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa 2=1 Ministries Australia Andronicus Kyuvu, kutoka Nchini Kenya alipokuwa akitoa semina ya kumkomboa mtanzania katika dimbwi la umasikini kwa lengo la kufungua ufahamu wa kufanya kazi.
Katika semina hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wchungaji,wanandoa na wajane Kyuvu amesema watu wengi wanaishi maisha ya kumtegemea Mungu lakini hawafanyi kazi jambo ambalo linawasababishia umasikini.

Amesema haiwezeka mtanzania akaendelea kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi wakati nchi ya Tanzania imejaa utajiri wa kila aina na njia pekee ni kufanya kazi kwa bidii.
Kutoana na hali hiyo amesema 2=1 Ministries Australia limekuja Tanzania kwa malengo ya kuwajengea uwezo wanandoa,wajane na baadhi ya viongozi wa dini jinsi ya kuandaa miradi ambayo itawatoa katika dimbwi la umasikini.
Kuhusu wanandoa, Kyuvu amesema ndoa nyingi zinavunjika kutokana na maisha duni jambo ambbalo linasababishwa na umasikini wakati kuna uwezekano mkubwa wa kufanya shughuli ndogo ndogo au kuandika miradi mikubwa kupitia vikundi na kuanzisha miradi ambayo inaweza kuwanufaisha.

Kwa upande wake mratibu wa Huduma hiyo nchini Tanzania, Dkt. Benson Rutta amesema huduma hiyo inalenga kuwainua watanzania wa kipato duni na kuzifanya ndoa kuimarika kiuchumi.
Amesema kwamba mpaka sasa mikoa mitano imefikiwa na huduma hiyo ukiwepo Mkoa wa Dodoma, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Geita huku akieleza kuwa Mwanza na Geita tayari wameisha anza kuwezeshwa kimitaji.
Amesema huduma hiyo inalenga kutoa elimu ya kufanya biashara kwa mtu mmoja mmoja na kufanya biashara kubwa ya kufungua viwanda vikubwa,kujenga hospitali,kujenga shule na huduma nyingini kwa sehemu ya taasisi.

Amesema watanzania wanatakiwa kujikwamua kimaisha kwa kufanya kazi kwani kwa sasa suala la kusubiri misaada kutoka kwa wazungu inaelekea kukoma badala yake kila mtu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii.