Na Lucy Lyatuu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Suleimani Jafo amesema taarifa ya hali ya ufanyaji biashara katika soko la Kariakoo Dar es Salaam kati ya wageni na wazawa imebaini mnyororo wa thamani wa biashara unafanywa na wageni.
Aidha alisema ipo haja ya kupitiwa upya kwa sera ya uwekwzaji nchini pamoja na kufanya mabadiliko ya sheria ili kuhakikisha wageni wanaokaa nchini wasifanye biashara zinazoweza kufanywa na wazawa.
Ripoti hiyo inatokana na Kamati iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan Februaei 2 ambapo Kamati ilimaliza kazi Maxhi 17 na kuwasilisha mapendekezo.
Akizungumza jana Dar es Salaam alipokutana na Kamati hiyo,wviongozi wa wafanyabiashara na waluu wa taasisi mbalimbali Jafo alisema Mambo mengine yaliyobainika ni kuwa watanzania wanatoa taarifa zao kwa wageni ili kutengeneza kampuni.
Alisema kupitia taarifa hiyo ipo haja ya kuhakikisha watanzania wanaendelea kufanya kazi bila kuathiri demokrasia.
Alusema kupitia taarifa ya ripoti hiyo kutakuwa kunafanyika tathmini kila baada ya muda kyangalia hali ya utekelezaji wa mapendekezobyaliyotolewa katika taarifa hiyo na kiwango kilichofikiwa.
“Kupitia tathmini hiyo ni ili kujua eneo fulani kulikuwa na changamoto gani na timu hiyo ya ufuatiliajia itaongozwa na makatibu wakuu ili kuona hatua zilizocvukuliwa zimefikia wapi.’, alisema.
Alisema viongozi pia watakuwa wanahakiki yale walitokybaliana na jinsi yanavyofanyiwa kazi kwa kywa Rais Samia anategemea suala hilo lipatiwe suluhu ya kudumu ili watanzania nao waweze kunufaikka.
” Taarifa hii iwe kioo kwa kila sekta nchi nzima, ” Alisema Jafo akitolea mfano sekta ya madini kuwa wachimbaji wadogo nao wamekywa wakitoa taarifa zao kwa wageni.
Alisema kupitia taarifa hiyo Watu 703 wamepewa adhabu mbalimbambali huku 257 wamefikisha taarifa zao za ukaazi, 4796 wameondoshwa nchini.
Alisema Kariakoo wageni 62 wameondolewa lengo kuisafisha iwe salama kwa wafanyabiashara iwe na manufaa kwa Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila alisema hali iliyopo sasa siyo nzuri kwani kuna tishio la wazawa kunyanganyana fursa kwa sababu ya uwezo mdogo wa uchumi hivyo kilichopo kwa sasa asilimia kubwa ya wageni hususani wachina n wengineo wanatumia majina ya wazawa.
Chalamila aliomba nia iwekwe mbele ili kulinda maslahi ya wazawa na wageni.
Akitoa taarifa ya Kamati hiyo Dkt.Suleiman Serera Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara
Alisema Hatua imeanza kuchukuliwa ambapo idara ya uhamiaji wamefanya ukaguzi maalumu wa wageni wanaoishi bila vibali nchini na waliobainika raia 7900 wamekamatwa.
Aidha alisema Brela wameanza kuzuia wageni wanaofanya biashara za wazawa huku ikifanya ukaguzi wa biashara kama zinafanana na za wazawa.