MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mawakili Wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Katiba Ya Nchi Wanapoandika Sheria
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mawakili Wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Katiba Ya Nchi Wanapoandika Sheria
Habari

Mawakili Wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Katiba Ya Nchi Wanapoandika Sheria

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu                                                            

ARUSHA:MWANDISHI Mkuu wa sheria nchini Tanzania, Onorius Njole amewakumbusha Mawakili wa serikali nchini kuzingatia Katiba ya nchi wanapoandika sheria au wanapotoa ushauri wa kisheria kwa serikali katika jambo lolote.

Mwandishi huyo Mkuu wa Sheria ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya pili ya mwaka ya Mawakili wa serikali nchini yanayoendelea Jijini Arusha na kuwakutanisha zaidi ya Mawakili 300 kutoka kila kona ya Tanzania.

“Katiba iongoze ushauri wowote mnaoutoa kwa Serikali katika jambo lolote linalohitaji ushauri wa kisheria kutoka kwenu kama Mawakili wa Serikali, lakini pia huwezi kuwa mshauri mzuri wa kisheria kama hujui mambo ya Muungano.

“Pamoja na kuwa mnatoa ushauri na Tafsiri kwa mujibu wa sheria kwa Serikali lakini lazima kuzingatia sera, mazingira na ajenda za nchi na dunia kwa wakati huo,” amesema.

Mwandishi huyo Mkuu wa Sheria nchini amesema kwa sasa Serikali inahamasisha uwekezaji, “kwa hiyo unapoletewa jambo utoe ushauri wakati unajua kuwa linakinzana na sera ya wakati huo sio vyema kuishia kusema kuwa sheria hairuhusu bali toa ushauri wa nini kifanyike kurekebisha sheria husika kama litakuwa na maslahi mapana kwa Taifa,”.

Njole amewasa mawakili hao wa serikali wanapotoa ushauri kwa kusema jambo fulani ni hatarishi kwa maendeleo ya nchi, basi ni vyema pia kusema namna ya kuzitatua ili kupata tija lifanyike kwa tija bila kuleta athari kwa nchi.

“Nyinyi kama Washauri wa Serikali kwenye masuala ya kisheria kwenye maeneo yenu lazima umjue mnayempatia ushauri, acheni kuandika maneno magumu na kuzunguka zunguka kwa maneno mengi, weka ushauri wako mwanzo tuu wakati mnashauri Mawaziri, Makatibu wakuu na viongozi wengine maana wana kazi nyingi hawawezi kuanza kusoma taarifa ndefu sana,” amesema.

Akichangia mada hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumu, Sirillius Matupa amewataka mawakili wa serikali hao wanapotoa ushauri wa Kisheria kuhakikisha ushauri wanaoutoa haupigi kelele.

“Mnapopewa jukumu la kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali kuhusu jambo lolote hakikisheni ushauri mnaoutoa haupigi kelele, maana tumeshuhudia nyakati fulani unapokea ushauri kutoka kwa mtaalamu wa sheria lakini kunakuwa na malalamiko na maneno mengi sana kuhusu ushauri huo na hivyo kusababisha mtoa maamuzi kupata shida kwenye kuutumia,” amesema.

Mafunzo hayo ya siku tano yanawakutanisha mawakili wa serikali kutoka kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwakumbusha mambo mbalimbali ambayo wanapaswa kuyazingatia wakati wanatekeleza majukumu yao ili waweze kutoa mchango chanya kwenye maendeleo ya taifa.

You Might Also Like

Afrika yatakiwa kutokuwa na Matabaka katika kutekeleza AFCFTA 

Watu Milioni 300 Afrika Kutumia Nishati Ya Umeme Ifikapi 2030-Biteko

𝐓𝐅𝐒 Y𝐚𝐧𝐝𝐚𝐚 M𝐤𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 W𝐚 M𝐢𝐚𝐤𝐚 1𝟎 Ku𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐳𝐚 N𝐚 K𝐮𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 M𝐢𝐬𝐢𝐭𝐮 Ya Mi𝐤𝐨𝐤𝐨 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐁𝐚𝐫𝐚

Japan Yatoa Bilioni 27 Kuboresha Sekta Ya Afya

Kongani za viwanda kutoa ajira nchini.

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Kombo: Ushirikiano Wa China, Tanzania Umeleta Maendeleo Ya Kijani
Next Article Miaka Minne Ya Samia, TANESCO Yajivunia Kudhibiti Upotevu Wa Umeme
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?