Na Waandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amepongeza mafanikio mema yaliyofikiwa na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Pongezi hizo amezitoa katika mahojiano yaliyofanywa na Waandishi wa Habari katika makala haya.
Waziri Kombo katika mahojiano hayo anasema, ushirikiano baina ya China na Afrika sio tu umekuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania, bali pia umechagiza matokeo chanya kwa Bara zima la Afrika.
Maendeleo ya kilimo cha kisasa yamesaidiwa na ushirikiano katika sekta ya miundombinu
Akizungumzia maendeleo ya kilimo cha kisasa kuwa yanasaidiwa na ushirikiano katika sekta ya miundombinu, anatolea mfano wa kilimo cha soya kwamba, umuhimu wa maendeleo ya miundombinu kwa ajili ya kilimo cha kisasa, umeongeza tija na mauzo ya soya nchini China.
Anasema kilimo cha kisasa kinahitaji mitambo, maendeleo ya kisasa na uboreshaji wa miundombinu, na hayo ni maeneo yanayohusiana sana na ushirikiano na China.
Anasema katika kushirikiana na China, Nchi ya Tanzania inaweza kuboresha hali ya usafiri na kupunguza gharama za usafirishaji, hivyo kuongeza ushindani wa soko la mazao ya kilimo.
Kombo anazungumzia hatua 10 za ushirikiano zilizotangazwa kwenye mkutano wa FOCAC. Ambazo zinashughulikia mahitaji muhimu ya Afrika, ikiwemo ustawi wa biashara, mnyororo wa viwanda, uunganishaji, kilimo, mambo ya afya, maisha ya watu na maendeleo ya kijani.
katika eneo la Ushirikiano wa maendeleo ya kijamii, Waziri Kombo anaweka mkazo Kwenye eneo la ubia kwa maendeleo ya Kijani.
Waziri Kombo ana imani juu ya mustakabali wa ushirikiano wa maendeleo ya kijani kati ya China na Afrika.
“China inaongoza duniani kwa teknolojia na soko katika sekta ya nishati inayotengeneza betri.
“China na Tanzania zinaweza kufanya ushirikiano wa kina katika mnyororo wa sekta ya betri, ili kutoa fursa zaidi za ajira za ndani na kukuza mabadilishano ya kiufundi,” anasema.
Naye Mwalimu wa lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) Ning Yi, anasema kuwa, Malengo sita ya maendeleo ya Kisasa na hatua 10 za Ubia zilizotangazwa na FOCAC 2024 zimetoa maarifa muhimu kwa ushirikiano wa Tanzania na China, hasa katika mambo ya mabadiliko ya kilimo na maendeleo ya kijani.
Ning anasema ushirikiano wa Tanzania na China katika kukuza kilimo cha kisasa unaonyesha umuhimu wa ushirikiano wa viwanda.
Kupitia maendeleo ya miundombinu na mitambo ya kilimo, tija na ushindani wa soko unaweza kuimarika.
Vilevile anasema katika ushirikiano katika sekta ya nishati hususan utengenezaji wa betri, uunganishaji wa rasilimali za madini ya Tanzania na teknolojia ya China utakuza maendeleo ya sekta mpya ya nishati ya pande hizo mbili na kuleta fursa za ajira na uboreshaji wa viwanda nchini Tanzania.
Mwandishi 1: Ye Tianfa, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: tianfa202123@163.com
Mwandishi 2: Ning Yi ni mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn