MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria
Habari

NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Danson Kaijage,

DODOMA: BARAZA  la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema limejipanga kuhakikisha linavuna magugu maji mapya katika ziwa Victoria.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Sware Semesi alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani kwa Waandishi wa Habari  katika ukumbi wa wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.

Amesema NEMC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na nchi jirani zinazopakana na Ziwa Victoria, wamefanya juhudi kuokoa ziwa hilo kutokana na kuibuka magugu maji mapya ambayo yanaweza kusababisha changamoto mbalimbali katika ziwa hilo.

Amesema kama magugu maji hayatavunwa yataitesa miundombinu katika ziwa hilo, kusababisha vivuko kuingiliwa maji na kukwamishaji uwekezaji unaofanywa katika ziwa hilo.

Pia amesema kwa miaka minne  ya 2020/21 hadi 2024/25, baraza hilo limeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi  na kufikia zaidi ya asilimia 68 ya malengo yaliyowekwa.

“Katika utekelezaji wa Miradi ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) baraza limesajili jumla ya miradi 8,058, kati ya hiyo 5,784 ni ya TAM na 2,274 ni ya Ukaguzi wa Mazingira.

“Vikao 3,836 vya wataalam vilifanyika kwa ajili ya kufanya mapitio  ya taarifa za TAM na Ukaguzi wa Miradi  na kutoa mapendekezo  ya maboresho  ya masuala ya msingi  ya kuzingatiwa  katika   taarifa  hizo.   Miradi 4,570 iliidhinishwa na kupewa vyeti vya mazingira.

“Kati ya hivyo, 3,058 ni vya TAM, 765 ni vya Ukaguzi, huku vyeti vingine vikiwemo vya kubadili masharti 169, vyeti vilivyohamishwa umiliki 552, vyeti vya muda (PEC) 53 na cheti kilichorudishwa,” amesema.

Ameeleza kuwa  Kabla ya mfumo Baraza lilikuwa linasajili takribani miradi 900  kwa mwaka na baada ya mfumo  Baraza linasajili  zaidi ya miradi 2,000  kwa mwaka, jambo ambalo aliawma ni mageuzi makubwa ya Serikali ya   awamu ya Sita.

“Vilevile, kaguzi zilifanyika katika maeneo 178 ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

“Zaidi ya Tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria,” amesema.

You Might Also Like

Matumizi Ya Baiteknolojia Nchini ni Madogo – Profesa Yanda

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani, Mwenyekiti wa CCM Pwani, wawanadi wagombea wa CCM

NIT yawapika vijana

Mabasi  Mapya Ya Mwendokasi Yaanza Kazi Njia Ya  Kimara, Gerezani na Kivukoni

Rais Samia akunwa na Tarura

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwanjala Wa TRC Aelezea Umuhimu Wa VETA
Next Article COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?