Na Mwandishi Wetu
DODMA: WAZIRIi wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Kenichi Ogasawara.
Maxungumzo hayo yamehusu kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ukuzaji ujuzi na teknolojia kwa vijana.

Ridhiwani amesema hayo leo Machi 21, 2025 Jijini Dodoma alipokutana na ujumbe huo kutoka nchini Japan.
Pia amesema kupitia programu ya ukuzaji ujuzi inayotarajiwa kuanzishwa baina ya nchi hizo mbili italeta tija kwa vijana kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaoupata kutoka nchini Japan.
Katika hatua nyingine Ridhiwani amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufungua mipaka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa watanzania kupata kazi nje ya nchi.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan, Ogasawara amesemaTanzania ni moja ya Nchi ya kipaumbele katika program hiyo ya mashirikiano ya ukuzaji ujuzi na teknolojia kwa vijana wa Kitanzania.
