Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MFUMO wa kumzuia mtumiaji wa choo asiweze kutoka baada ya matumizi mpaka atakapo ‘ flash’ ndipo mlango utafunguka, umetengenezwa ili kuimarisha usafi chooni.
Mkufunzi wa Chuo cha Al- Maktoum (AMCET), Nyazara Haji ameeleza hayo alipozungumza na Mfanyakazi Tanzania katika Maadhimisho ya miaka 30 ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ikiwa ni siku ya pili katika Kituo cha Kimataifacha Mikutano cha Julius Nyerer Dar es Salaam (JICC).

” Kupitia mfumo huo amesema ukidumbukiza Sh 500 mlango utafunguka ukiingia unajifunga. Utafanya shughuli zako ukimaliza, unaflash ndiopo mlango utafunguka,” amesema.
Amesema kwa kufanya hivyo usafi wa choo utaimarika.

Akielezea teknolojia hiyo amesema mtumiaji atalipia fedha hata kama hakuna mtu anayepokea kwa kudumbukiza Sh 500 kwenye mashine ndipo mlango utafunguka.
Amesema mara nyingi kwenye vyoo vya jumuiya watu wengi hutumia choo bila kusafisha.