Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAFUGAJI wa wanyama wanaokula majani wakiwemo ng’ombe wamekumbukwa na kutengenezewa mashine ya kuchakata chakula cha mifugo yao hususan majani.
Mwalimu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Mikumi mkoani Morogoro Peres Shao, amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 30 ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA), yanayoendelea kwa siku ya pili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salqam ( JICC).

Shao amesema wamebuni mashine hiyo baada ya kuona changamoto ya mfugaji anakata majani kwa kutumia panga na kigogo.
” Hiyo ndiyo imetufanya tubuni mashine hii ili ifanye kazi kwa urahisi inatumiwa na mtu yeyote mwenye akili timamu,” amesema.
Amesema katika mashine hiyo ndani kuna mapanga mtu asipokuwa makini itamkata violent.
Amesema mashine hiyo waliyoibuni ina uwezo wa kukata kilo 500 kwa saa moja.
Amesema chuo chao wapo Dar es Salaam kuadhimisha miaka 30 ya VETA.
Amewashauri wazazi kuwapeleka vijana kwenye Vyuo vya VETA ili wapate ujuzi utakaowasaidia kwa maisha ya baadaye.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Antony Kasore amesema wataendelea kutoa elimu ya ufundi stadi pamoja na kusimamia bunifu na teknolojia mbalimbali.
.