Na Danson Kaijage.
DODOMA: MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF umejipanga kutoa mafao kwa mstaafu siku moja baada ya kupewa barua yake ya kustaafu badala ya kusubiri kulipwa mafao yake kwa siku 60 tangu kustaafu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mashomba, alipotoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, kwa miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mashomba amesema hiyo ni kutokana na juhudi na umakini wa mfuko kuhakikisha wastaafu ambao ni wachangiaji wakuu wa mfuko huo wanapostaafu hawapati shida.
Amesema kwa sasa mfuko huo unatoa mafao ndani ya siku 30 tangu anapostaafu mtumishi.
Amesema juhudi za serikali ikiwepo mashirikiano mema na watumishi imewawezesha mfuko huo kuongeza wanachama wapya wanaochangia mapato.
Amesema wanachama wapya 1,052,176 wameandikishwa Katika kipindi cha miaka minne kilichoanzia Machi 2021 mpaka Februari 2025.