Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: ” TUNAHITAJI sana kuimarisha ushirikiano baina ya viwanda na wazalishaji,”.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema hayo leo Machi 14, 2025 wakati wa Kongamano na Wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Kongamano hilo limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA.
Amesema kwa kufanya hivyo VETA ijenge mahusiano na wazalishaji mbalimbali wakiwemo wa magari.
“Tungetaka kuona ushirikiano wa kampuni za ujenzi na VETA, ujenzi wa nyumba nzuri na hivi sasa ujenzi wa nyumba nzuri unaenda kasu sana,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore amesema kwenye eneo la ujuzi wana jukumu la kufundisha ujuzi.
Amesema kwa kuthamini ujuzi serikali inahakikisha vyuo vya ufundi vinakuwepo vya kutosha, ndio maana vipo zaidi ya 800 nchini.
“Maana yake ni sekta ambayo watu wengi wanahitaji kupata ujuzi,” amesema.