MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ujenzi Wa Maabara Tatu Za Sayansi Kuanza, OUT Yasaini Mkataba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Ujenzi Wa Maabara Tatu Za Sayansi Kuanza, OUT Yasaini Mkataba
Makala

Ujenzi Wa Maabara Tatu Za Sayansi Kuanza, OUT Yasaini Mkataba

Author
By Author
Share
5 Min Read

Na Lucy Ngowi

KATIKA siku za karibuni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kilisaini mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Elimu ya Juu Tanzania kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET).

Utiaji saini huo ni hatua muhimu katika juhudi za Serikali za kuboresha elimu ya juu na kuimarisha mazingira ya kujifunza na kufundishia nchini.

Kwa kuwa mradi huo wa kuboresha elimu ya juu nchini Tanzania unasaidia ukuaji wa uchumi kwa kuimarisha vyuo vikuu, utafiti na ujuzi wa wanafunzi katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Makamu Mkuu wa OUT, Profesa Elifas Bisanda anasema chuo hicho kimesaini mkataba  wa ujenzi wa maabara tatu na Mkandarasi Arm Strong Int. Ltd, ambao utakuwa ni wa miezi nane.

anasema mkataba huo uliosainiwa wa ujenzi wa maabara hizo upo chini ya chuo hicho kupitia Mradi wa HEET.

Anasema mradi wa HEET hauwezi kuwa wa maana kama vitafanyika vitu ambavyo havitaleta mabadiliko katika jamii.

“Uwepo wa mradi huu ni sehemu ya maeneo saba ya utekelezaji wa HEET. Tunalenga kujenga maabara za kisayansi, tunatambua nchi haiwezi kuendelea au kubadilika bila kuweka msisitizo kwenye sayansi,” anasema.

Anasema mkandarasa waliyeingia naye mkataba atajenga maabara tatu katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Kigoma. Maabara nyingine zilizobakia zitajengwa na wakandarasi tofauti tofauti.

Naibu Makamu Mkuu wa OUT upande wa Taaluma, Tafiti na Huduma za ushauri. Profesa Alex Makulilo anasema mradi huo unaotekelezwa na chuo hicho kwa thamani ya dola milioni tisa.

Anasema fedha hizo zimegawanyika katika vipengele mbalimbali , kwani asilimia 75 ya mradi mzima zinaenda kwenye ujenzi, maabara saba katika Kanda saba.

Anasema mradi huo ni sehemu ya mpango wa Serikali unaotekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ili kuimarisha elimu ya juu kupitia uwekezaji katika miundombinu, teknolojia na rasilimali watu.

Anasema chuo kikuu huria ni miongoni mwa taasisi 22 za elimu ya juu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Katika kutekeleza mradi huu OUT kimetengewa Dola za Kimarekani milioni tisa na unalenga kupanua na kuboresha mazingira ya kujifunzia, ikijumuisha

kuimarisha miundombinu ya kidijitali, rasilimali za mtandaoni, kujenga uwezo wa kitaaluma, na kuwanoa wafanyakazi katika mbinu za kisasa za ufundishaji, utafiti na ubunifu.

“Mradi huu pia una lengo la kupunguza pengo la kijinsia katika masomo ya sayansi na teknolojia kwa kuwawezesha wanawake kushiriki kwa wingi katika programu za STEM.

“Tunatambua kuwa maendeleo ya taifa lolote yanategemea rasilimali watu wenye ujuzi wa hali ya juu, hususan katika nyanja za sayansi na teknolojia, hivyo uwekezaji huu ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu,” anasema.

Anasema OUT kitajenga majengo saba katika mikoa ya Arusha, Mwanza,Kigoma, Morogoro, Pwani, Mtwara na Njombe kwa matumizi mbalimbali, kila jengo litakuwa na maabara sita za sayansi katika kila moja ya vituo saba vya kikanda .

Anasema kila kituo kitahudumia angalau mikoa mitatu., na kwamba maabara hizo zitatumika kama sayansi katika maeneo ya kipaumbele ya mradi.

Anasema pia majengo hayo yatakuwa na kituo cha TEHAMA, sehemu ya mafunzo ya vitendo kwa ukarimu na utalii, pamoja na maghala ya kuhifadhia vifaa na ofisi kwa wafanyakazi wa maabara.

Anasema chuo kinaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya elimu kama nyenzo kuu ya maendeleo. Kupitia mradi huo wa HEET wanaamini utasaidia kuongeza fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kupata elimu yenye ubora wa kimataifa.

Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Kampuni ya Arm Strong Int. Ltd, Pastory Masota anasema wakandarasi ni watekelezaji wa mradi ukiooitia michakato mingi, kupitiwa na watu wengi.

Anasema wao wataweka yote waliyokubaliana katika hali halisi.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Profesa Joseph Kuzilwa anasema kuna uhusiano mkubwa kati ya uwekezaji wa elimu na ukuaji wa uchumi.

 

 

 

You Might Also Like

Kinywaji Cha China Chavuka Mipaka Chatua Tanzania

OSHA yaelimisha sheria mahala pa kazi kwa JOWUTA

Dkt. Biteko Afuta Likizo Za Watumishi Wote Tanesco

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article JKCI Imeona Wagonjwa Zaidi ya Laki Saba Kwa Miaka Minne
Next Article Stamico Yapewa Tuzo Na FDH Kujali Wenye Ulemavu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

JAB Yaanza Rasmi Kutoa Vitambulisho Kwa Waandishi Wa Habari
Habari May 19, 2025
Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili
Habari May 19, 2025
Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii
Habari May 19, 2025
Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card
Habari May 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?