MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Elimu Ya Fedha Yafika Makanya Same
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Elimu Ya Fedha Yafika Makanya Same
Habari

Elimu Ya Fedha Yafika Makanya Same

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Danson Kaijage
KILIMANJARO: SERIKALI imepeleka elimu ya fedha kwa wananchi wa Kata ya Makanya, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, itakayochochea maendeleo yao kiuchumi.
Elimu hiyo ya fedha inawalenga wananchi, wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima, wafugaji, watumishi wa umma na binafsi, watoa huduma za fedha kuwawezesha kufahamu sheria, kanuni na miongozo ya huduma ndogo za fedha.
Vile vile kufahamu masuala ya akiba, mikopo, uwekezaji wa fedha, bima, matumizi bora ya fedha na kujipanga na maisha ya uzeeni.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Dionesia Mjema, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha.
Vile vile kupanga bajeti, kuweka akiba, na mikopo salama.
“Matatizo mengi ya kifamilia hutokana na changamoto za kifedha, hivyo elimu hii itasaidia kuboresha maisha ya familia nyingi, na ndoa nyingi zinazovunjika hutokana na mzigo wa madeni.
“Nahimiza ushirikiano kati ya wanandoa katika kupanga matumizi ya mikopo,” amesema.
Diwani wa Kata ya Makanya,  Damari Kangalu ametoa shukrani kwa Wizara ya Fedha kwa kuwapelekea mafunzo hayo muhimu, kwa kuwa elimu hiyo itawasaidia kuepuka mikopo umiza na kuimarisha hali yao ya kifedha.
“Hata wale wenye kipato kidogo wanaweza kuweka akiba na hatimaye kuwekeza ili kupata faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Hili litasaidia kuinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla,” amesema .
Ofisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Stanley Kibakaya, ameeleza kuwa wapo watoa huduma za fedha wasio waaminifu na hawatoa taarifa sahihi za huduma zao kwa wateja hali hiyo imesababisha watumiaji wengi kutojua wajibu wao na kusababisha migogoro kati yao.
” Hivyo kila Mtoa huduma ahakikishe kabla ya kutoa huduma wanatoa elimu ya fedha na kuweka wazi wajibu wa Mtoa Huduma na Mteja kwenye mkopo au huduma anayotoa,” amesema.
Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Makanya wamefurahishwa na mafunzo hayo yanayotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake kwa kuratibu elimu hiyo muhimu.
Mafunzo hayo yanatolewa katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro, zikiwemo Wilaya ya Same, Mwanga na Rombo.

You Might Also Like

Madini Yaweka Rekodi Makusanyo Ya Maduhuli

TEA Mshindi wa Kwanza Maonyesho Ya Mfuko wa Utamaduni

DAWASA na TARURA Kuendeleza Ushirikiano Ulinzi wa Miundombinu

Dodoma Yazizima Wakati Samia, Nchimbi  Wakichukua Fomu Ya Urais

Wizara ya Nishati Yajivunia Jitihada Katika Kulinda Haki, Usawa na Kuwawezesha Wanawake

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Samia Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu ALAT
Next Article Kiswahili Kimeanza Kubanangwa- Kabudi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?