MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Matwebe Aipongeza Serikali Kushirikisha JUMIKITA  Kwenye Shughuli Za Kitaifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Matwebe Aipongeza Serikali Kushirikisha JUMIKITA  Kwenye Shughuli Za Kitaifa
Habari

Matwebe Aipongeza Serikali Kushirikisha JUMIKITA  Kwenye Shughuli Za Kitaifa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imewapatia waandishi wa habari wa mtandaoni nafasi kubwa ya kushiriki katika shughuli za kitaifa, tofauti na ilivyokuwa awali.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Kimtandao Tanzania (JUMIKITA), Shaabani Matwebe, amesema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na Star TV.
Matwebe amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imetoa nafasi kwa JUMIKITA kwa kuwawezesha kushiriki katika matukio muhimu ya kitaifa, ikiwemo misafara ya viongozi wakuu wa serikali.
“Katika kitu ambacho niipongeze Serikali ya Awamu ya Sita ni kwamba sisi baada ya kuunda jumuiya na kutafuta njia mbalimbali za kushirikiana na serikali, tumepokelewa vizuri.
“Waandishi wa habari wa mtandaoni sasa wanashiriki katika misafara mikubwa ya viongozi, jambo ambalo zamani halikuwepo,” amesema.
Ameongeza kuwa, awali kabla ya kuanzishwa jumuiya hiyo 2021,
waandishi wa habari wa mtandaoni walikumbwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kutotambuliwa rasmi na taasisi za serikali.
Amesema jitihada kubwa zimefanyika hivi sasa waandishi wa habari za mitandaoni wanatambuliwa katika sekta ya habari.
Kwamba kuoitia JUMIKITA, waandishi wengi wa habari wa mtandaoni wamepata mafunzo ya maadili ya uandishi wa habari, wengine wakipata fursa ya kushirikiana na taasisi za serikali na sekta binafsi.
Ameagiza wanajumuiya hiyo kuzingatia weledi na maadili katika kazi wanazozifanya.
“Sera za serikali ni nzuri, na toka Awamu ya Sita imeingia madarakani, tumeweza kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
“Hata hivyo, waandishi wa habari wa mitandaoni wanapaswa kuwa makini, kufuata maadili na kuhakikisha wanatoa habari sahihi na zenye ukweli,” amesema.
JUMIKITA inaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kuhakikisha waandishi wa habari wa mtandaoni wanapata mazingira bora ya kazi, fursa za mafunzo na ulinzi wa haki zao.

You Might Also Like

Biteko – Asisitiza Umuhimu Wa Mifumo Thabiti Ya Nishati Jadidifu Kukidhi Mahitaji Ya Nishati

Sekta Ya Madini Yapaisha Pato La Taifa

Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF

Stamico Yapewa Tuzo Na FDH Kujali Wenye Ulemavu

Uzinduzi wa Ubia Wiki Ya Ubunifu Tanzania 2025 Wafanyika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Askari Wawili wa JWTZ Wafariki, Wanne Wajeruhiwa DRC
Next Article Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Wanawake Jijini Arusha
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?