MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kanisa Lawashika Mkono Shule Ya Msingi Kibamba, Halmashauri Ya Ubungo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kanisa Lawashika Mkono Shule Ya Msingi Kibamba, Halmashauri Ya Ubungo
Habari

Kanisa Lawashika Mkono Shule Ya Msingi Kibamba, Halmashauri Ya Ubungo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: KANISA  la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, limetumia Sh. Milioni 470.8 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika Shule ya Msingi Kibamba iliyopo Halmashauri ya Ubungo Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Genuine Kahatano amesema hayo katika taarifa yake ya shukrani aliyoisoma kwa uongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa serikali, walimu pamoja na wanafunzi, muda mfupi kabla ya kukabidhiwa miundombinu hiyo.
Kahatano ametaja miundombinu hiyo iliyojengwa na kukarabatiwa kuwa ni
vyumba vya madarasa tisa vikiwa na umeme, ofisi mbili ndogo za walimu na Ofisi moja kubwa ya walimu.
Pia vyoo vya wanafunzi na mnara wa matenki ya maji kwa thamani ya sh milioni 329.5.
“Shule ya msingi Kibamba, tunatoa chozi la furaha tukisema asanteni sana kwa kazi kubwa isiyo na mfano mliyoifanya. Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki kwa kazi nzuri,”amesema.
Naye Rais wa Kanisa hilo, Juventinus Rubona amesema miradi iliyokamilika imegharimu Sh. Milioni 753.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni wa shule hiyo ya Kibamba, Kituo cha Afya Kimara na Kituo cha Afya Makuburi.
Amesema miradi ya sasa inayotarajiwa kukamilika ina thamani ya Sh. Milioni 522.
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ya Ubungo, Hassan Mkwawa amelishukuru Kanisa hilo kwa msaada walioutoa katika shule hiyo na maeneo mengine.
Ameagiza miundombinu hiyo itunzwe ili kizazi kijacho kiweze kuitumia.

You Might Also Like

Maeneo ya hifadhi yalindwe na kutunzwa – Rais Samia

Maziwa Kukuza Uchumi Wa Wafugaji

LATRA CCC Yatoa Angalizo Uhitaji Mkubwa Wa Wasafiri Mwisho Wa Mwaka

ATCL Yaanzisha Safari Za Moja Kwa Moja, Dubai Na Zanzibar

Majaliwa: Anwani Za Makazi Kupunguza  Safari Kwa Viongozi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dar es Salaam Kuunda Kamati Ya Kupitia Majengo Chakavu
Next Article Muswada Wa Marekebisho Ya Sheria Za Kazi 2024 Wapitishwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Habari April 29, 2026
Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Habari April 28, 2026
NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari April 27, 2026
TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi
Habari April 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?