MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Vipima Ulevi Zaidi Ya 3000 Vyakabidhiwa Polisi Na Latra
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Vipima Ulevi Zaidi Ya 3000 Vyakabidhiwa Polisi Na Latra
Habari

Vipima Ulevi Zaidi Ya 3000 Vyakabidhiwa Polisi Na Latra

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: VIFAA 3,050 vya kupima ulevi kwa madereva vimetolewa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa Jeshi la Polisi nchini kwa ajili ya kusaidia kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi na wazembe, pale wanapoendesha pasipo kuzingatia sheria.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura akipokea vifaa hiyo amesema, jeshi hilo limeweka mikakati madhubuti ya kudhibiti ajali za barabarani ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyokuwa akiyatoa mara kwa mara ya kuhakikisha ajali za barabarani zinadhibitiwa ipasavyo.

Wambura amesema kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani watakuwa wakali kwa madereva wazembe ambao wamekuwa wakisababisha ajali za barabarani ikiwa ni Pamoja na kutoa elimu hiyo kwa jamii ili kuhakikisha watanzania wanakuwa salama.

“Tumeweza kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali na sasa nguvu pia tunazielekeza kwenye usalama barabarani kwa kuwa takwimu za ajali bado zipo juu hivyo ni lazima tuwe wakali sana ili kuona sheria za usalama barabarani zinafuatwa ili kuokoa maisha ya Watanzania,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo amesema utendaji kazi wa mamlaka hiyo unahitaji ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye dhamana ya kusimamia Sheria za Usalama barabarani.

Amesema vipima ulevi hivyo vitasaidia kikosi hicho kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi na wazembe pindi wanapokuwa barabarani na kuendesha pasipo kuzingatia sheria.

Suluo amesema uwepo wa vifaa hivyo utasaidia kupima madereva mara kwa mara wawapo barabarani jambo ambalo litasaidia kufanya barabara  kuwa salama.

Pia amesema mamlaka hiyo itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutumia mifumo katika kufanya ukaguzi wa magari ambapo kwa sasa wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali.

You Might Also Like

  Tanesco Yagawa Zawadi Ya Majiko Sabasaba Kuhimiza Matumizi Nishati Safi

Uzinduzi wa Ubia Wiki Ya Ubunifu Tanzania 2025 Wafanyika

TFS Yashiriki Maonesho ya Nane ya Madini Geita

VETA Yapaa Miaka Minne Ya Rais Samia

Vyombo vya Habari ni Kama Maji’ -Biteko 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Madereva Mabasi YA Kukodi Waitwa LATRA Kabla YA Januari 12, Mwaka Huu
Next Article Nchemba Afungua Mafunzo Ya PAC
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?