JANUARI 3, 2024: Bi mdogo apigwa, alishwa kinyesi
MKAZI wa Buchegera, Serengeti Nyaikongoro Ntumbo (28), anatuhumiwa kumpiga mkewe mdogo na kumlazimisha kula kinyesi.
Mwathirika wa tukio hilo, Eliza Nchagwa (20) amesema tukio hilo limetokea Novemba 21, mwaka jana.
“Mume wangu alinipiga sana hadi nikajisaidia haja kubwa. Akachukua panga, akaniamuru nile kinyesi na nisipofanya hivyo ataniua.
“Sikuwa na cha kufanya kwa kweli, nililazimika kula hadi kumaliza. Kipigo kiliniacha na maumivu makali ya tumbo na mwili,” anasema Eliza kwa sauti ya simanzi.
JANUARI 9,2024 Mume adaiwa kuua mke, akimkata kichwa,viungo
POLISI Wilayani Makete, Mkoani Njombe inamshikilia Juma Kyando (36) kwa tuhuma za mauaji ya mkewe Tumaini Luvanda.
Inadaiwa mtuhumiwa alimchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, kisha inadaiwa aliukata mwili huo vipande vipande na kutupa baadhi ya viungo kwenye mto, vingine jirani na nyumba yake.
FEBRUARI 2, 2024: Mjamzito wa mapacha miezi nane achinjwa
Mumewe amtoboa tumbo, atoa mapacha awaua, amkatakata mmoja ampike kama kitoweo, aua mtoto wake mwingine wa miaka miwili
SEPTEMBA 7, 2024: Kifo cha utata – ni kada wa chadema aliyedaiwa kutekwa Ali Kibao
JESHI la Polisi limethibitisha taarifa za kuuawa kwa kiongozi wa Chana cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Ally Kibao.
‘’Jana Septemba 7,2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kushushwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na watu ambao hawakuweza kutambulia na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo. Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambuliwa kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulizi umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao.’’ Inaeleza taarifa ya jeshi hilo.
OKTOBA 29, 2024: Baba adaiwa mahari baada ya mwanae kutomzalia mumewe
NOVEMBA 8,2024: Adaiwa kumlewesha mwanafunzi wake , akambaka darasani
NOVEMBA 14, 2024: Tukio la utekaji Dar, laacha maswali tele, mashuhuda wasimulia waliyoyaona, kuyasikia eneo la tukio, mfanyabiashara Tarimo alivyojinasua- Polisi yaanza uchunguzi
Disemba 8, 2024 Mfamasia auawa, mume ahusishwa
MWILI wa mfamasia wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, Magdalena Kaduma umekutwa umefukiwa pembezoni mwa nyumba aliyokuwa akiishi huku sababu ya kifo chake ikiwa haijulikani na mume akishikiliwa na polisi.
Inadaiwa kuwa tangu alipoondoka nyumbani kwake Desemba 4, mwaka huu kuelekea kazini kwake, hakuonekana nyumbani hadi juzi saa 9:00 alasiri ndugu zake na wajumbe wa Mtaa Hondogo, Kata ya Kibamba, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam walipobaini mwili wake ukiwa umefukiwa meta 15 kutoka ilipo nyumba yake.
Imeandaliwa Na Lucy Ngowi