Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MRADI wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT), umekuwa ni sehemu muhimu ya urafiki wa China na Tanzania, wenye kutoa mchango mkubwa katika uchumi, maendeleo na uboreshaji wa maisha.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Usalama Tawi la Tanzania, kutoka Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC), Li Yuling wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya Jiao Zhu China -Tanzania.
Amesema mradi huo wa BRT, awamu ya nne sehemu ya tatu ni sehemu muhimu ya urafiki wa China na Tanzania, na kwamba sio tu unaboresha usafiri wa umma wa Dar es Salaam ambao ni mji mkuu wa Tanzania, lakini pia unatoa mchango mkubwa katika uchumi.

“Mradi huo unajumuisha ujenzi wa vituo muhimu vya usafiri, vituo vya mabasi na vifaa vingine vya trafiki. Unalenga kuboresha ufanisi wa usafiri wa mijini, kupunguza msongamano na kuimarisha hali ya usafiri ya wakazi wa eneo hilo,” amesema.
Amesema wameita waandishi wa habari kuonyesha watanzania juu ya dhamira ya makampuni ya Kichina katika maendeleo ya miundombinu inayoyafanya.
“Ili kuendeleza mafanikio hayo na kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, kampuni ya ujenzi ya China tawi la Tanzania imekutana na waandishi wa habari, kuzungumzia mafanikio hayo,” amesema.

Mwakilishi wa Mkandarasi katika mradi huo, You Xudong amesema mradi huo unaoendelea katika eneo la Kivukoni, utachukua miezi 18.
Amesema wanajenga jengo la ulinzi, choo, jengo la tiketi namba moja na jengo la tiketi namba mbili.
Naye Alvin Rujweka, Mwalimu kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT), amesema wamekuwepo na wanafunzi wao wanaosomea uhandisi kwa ajili ya masomo ya vitendo katika kampuni hiyo ya kichina ya CCCC.
Amesema anafundisha ujenzi wa kutumia matofali, mawe na ufundi bomba.
“Wanafunzi wanaoandaliwa kuwa wahandisi, wanapewa elimu ya vitabu na vitendo. Njia nyingine tunawapeleka kwenye miradi mbalimbali inayoendelea nchini, tunawaunganisha na soko kupitia fani walizosomea, ” amesema.
Mhitimu wa Diploma DIT mwaka huu 2024, Benson Mbilinyi amesema amepata nafasi ya kujiunga na kampuni hiyo ya CCCC, anafanya kazi kama msaidizi wa mhandisi.
Amesema ametumia elimu yake ya chuo akichanganya na uzoefu wa vitendo anaoupata katika kampuni hiyo.
Ameshauri wanafunzi kujitokeza kwenye fursa kwani yeye mara ya kwanza alikutana na kampuni hiyo ilipokwenda chuoni kwao kuonyesha utendaji kazi kwa vitendo,