Na Mwandishi Wetu
DODOMA: CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), kimetia saini ya Mkataba wa ujenzi wa jengo lake la Kitega Uchumi, sambamba na kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dodoma.
Hafla hio fupi imehudhuriwa na Wajumbe wote wa Baraza Kuu la TUGHE wakiongozwa na Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Joel Kaminyoge aliyeambatana na Viongozi wengine wa Kitaifa wa Chama, Watendaji, Viongozi Wastaafu, Wataalamu wa Ujenzi pamoja na Mkandarasi aliyepewa kazi ya Ujenzi wa Jengo hilo.

Jengo hilo litakuwa na Ofisi za Makao Makuu ya Chama pamoja sehemu ya Hoteli ya kisasa ambapo itakapokamilika itakuwa ni sehemu ya Kitega Uchumi kitakachoongeza mapato ya Chama.