MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watanzania Washauriwa Kula Senene, Kumbikumbi, Msusa, Ngogwe Kuepuka Udumavu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watanzania Washauriwa Kula Senene, Kumbikumbi, Msusa, Ngogwe Kuepuka Udumavu
Habari

Watanzania Washauriwa Kula Senene, Kumbikumbi, Msusa, Ngogwe Kuepuka Udumavu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: WATANZANIA wameshauri kula vyakula vya asili wakiwemo senene, kumbikumbi, msusa, ngogwe na vinginevyo ili kupata mlo kamili, kuepuka udumavu.

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Germana Leina amesema hayo wakati akichangia mada katika Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamoja na maonesho lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) lililomalizika hivi karibuni.

Katika kongamano hilo ametoa mchango unaohusiana na lishe katika mada iliyoeleza ni namna gani inaweza ikatumika elimu ya zamani, kimila au kitamaduni katika kutatua changamoto za lishe.

Amesema watanzania wakila vyakula hivyo vya asili vitasaidia kukidhi au kujaza pengo lililopo katika masuala ya lishe.

“Tafiti nyingi zinazofanywa zinazungumzia kwamba vyakula vya kitanzania huwa ni vya aina moja tu, yaani asilimia kubwa ya nishati lishe imetokana na kundi moja la vyakula ambavyo mara nyingi ni vile ambavyo vinatokana na nafaka mizizi na jamii ya ndizi mbichi, hivyo ni muhimu kutumia vyakula vya kizamani au vya kimili kama senene, kumbikumbi, msusa, ngogwe,” amesema.

Amesema wakishirikiana wanasayansi wa sasa pamoja na wale waliokuwa na ufahamu wa mila na tamaduni za makuzi ya chakula wanaweza wakaja na chakula ambacho kina lishe bora zaidi, kitakachokidhi mahitaji ya kilishe.

“Kama mnavyofahamu asilimia  30 ya watanzania wana udumavu, kwa bahati mbaya wengi wa hawa watoto wetu wako katika Kanda ambazo zinazalisha sana.

“Inawezekana kabisa chakula kinacholimwa ni cha aina moja tu na hivyo wakiweza kuongeza upatikanaji wa vyakula mbadala au vya kitamaduni tutaweza kuvuka hili pengo ambalo lipo la kilishe,” amesema.

You Might Also Like

Wanafunzi Shule Ya Anlex, Walimu Wao Watinga Bungeni

AUWSA Kutibu Maji Taka Yatumike Kwenye Kilimo

Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu

Matwebe Aipongeza Serikali Kushirikisha JUMIKITA  Kwenye Shughuli Za Kitaifa

TEA Yakabidhi Miradi Iliyokamilika Wilayani Mtama, Masasi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TAFIRI Wakabiliana Na Mabadiliko Ya Tabianchi
Next Article Tunatatua Malalamiko Ya Wateja – Kaguo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?