MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wamiliki Migodi Wapewa Siku 30 Kufanya Usajili
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wamiliki Migodi Wapewa Siku 30 Kufanya Usajili
Habari

Wamiliki Migodi Wapewa Siku 30 Kufanya Usajili

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
RUVUMA: WAMILIKI, Waendeshaji wa Migodi, Vituo vya Kuuzia na Kuhifadhia Makaa ya Mawe wamepewa siku 30, wawe wanasajili miradi yao  ili  kupata vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM).
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa muda wa usajili huo na uhakiki kuanzia Disemba nane mwaka huu, 2024
Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Jamal Baruti ametoa agizo hilo kutokana na  ukaguzi uliofanyika katika vitalu mbalimbali vya migodi na kubaini makosa yanayokiuka Sheria ya usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004.
Agizo hilo amelitoa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kukamilisha ukaguzi huo.
Ametaja makosa yaliyoonekana kuwa ni  kutofanyika kwa Tathmini ya Athari za Mazingira (TAM), ukosefu wa mifumo ya usimamizi wa mazingira, kutelekezwa kwa migodi pasipo kukarabati mazingira na uchafuzi wa vyanzo vya maji na hewa.
Pia kuongeza mawanda ya shughuli za migodi bila taarifa na idhini ya kisheria, kukosekana kwa taarifa za Upelembaji za kila mwaka na kukosekana kwa mipango ya urejeshaji Mazingira.
Amesema ukaguzi huo uliofanywa na timu ya wataalam kutoka NEMC kwa kushirikishana na wamiliki wa migodi umefanyika katika migodi 16 kati ya 18, maeneo ya biashara za makaa ya mawe saba kati ya 15 na maeneo mawili ya utafiti kuanzia Novemba 27 hadi Desemba nane, mwaka huu 2024 katika Wilaya za Madaba, Songea, Nyasa na Mbinga Mkoani Ruvuma.
Amesema timu hiyo pia imetoa elimu elekezi kwa wamiliki wa migodi ikiwemo kuweka miundombinu ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira, na  ukarabati endelevu wa mazingira,
Baruti amesema baraza hilo litaendelea kutoa maelekezo na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wamiliki wa migodi ili kuhakikisha uzingatiaji wa Sheria na utekelezaji maagizo yaliyotolewa.
Pia kuchukua hatua za kisheria kwa wadau wote watakaoshindwa kutekeleza maelekezo hayo ikiwa ni pamoja na kupewa adhabu au kusimamisha shughuli zao ili kulinda Mazingira, afya ya jamii na kuhakikisha uwiano wa maendeleo ya kiuchumi, uhifadhi wa Mazingira  na rasilimali za taifa.

You Might Also Like

Waziri Ridhiwani Awataka Wafanyakazi Kuongeza Bidii Katika Kazi

Benki Ya Dunia Kujenga Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa KV 400  Kutoka Uganda-Tanzania  

Tumeridhika na kazi za TTCL – Mwanaisha

Spika Ahoji Mwongozo Wa Wanaojitolea Kazin

Washauri Serikali Kutumia Fedha Za Miradi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali
Next Article Nishati Safi Ya Samia Yawafikia Wanawake chalinze
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?