Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MATUMIZI za Baiteknolojia nchini bado ni madogo ikilinganishwa na nchi zinazoendelea.
Baiteknolojia ni teknolojia za kisasa zinazojumuisha teknolojia ya uhandisi jeni (GMO), uzalishaji kwa njia ya chupa (tissue culture) na nyinginezo.
Profesa Pius Yanda kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amesema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu mchango wa Sayans, Teknolojia na Ubunifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mada hiyo ameiwasilisha katika kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamoja na maonesho linalomalizika leo jijini Dar es Salaam.

Ametaja sababu zinazochangia matumizi ya baiteknolojia kuwa madogo ni kutokuwa na teknolojia ya kutosha inayoweza kutumika ili itumike kwa uangalifu.
” Kitu kizuri tulichonacho Tuna misitu mingi, Tuna maliasili nyingi ambazo tunaweza kusema ni malighafi tunatakiwa kutumia kwenye hiyo baiteknolojia.
” Na baiteknolojia inatumika katika maeneo mengi ikiwemo afya, kilimo na mengineyo,” amesena.
Ameongeza kuwa kuna kila sababu ya kuhakikisha kunakuwa na ubunifu wa ziada kuhakikisha inawezekana kutumia teknolojia hiyo ya baiteknoloji kwa kiasi kikubwa zaidi.

Yanda ambaye amebobea kwenye masuala ya usimamizi maliasili, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi amesema teknolojia ya uhandisi jeni sasa hivi inaonekaba kuwa na mchango mkubwa katika uchumi pia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ameelezea fursa zinazotoa nafasi nzuri ya kuweza kushiriki kikamilifu katika kutumia hiyo baiteknolojia kwa ajili ya maendeleo ya leo, kesho na uchumi kwa ujumla.
Ffursa hizo ni pamoja na ushirikiano wa kimataifa na nchi mbalimbali ikiwemo nchi zilizoendelea hasa katika utafiti.
” Hayo nimaeneo ambayo tukiyafanyia kazi vizuri na wenzetu tutaenda kupata teknolojia bora zaidi.
“Changamoto kubwa tuliyonayo tunakabiliana na mabadiliko ya tabianchi, tunaathirika zaidi kuliko mabara mengine. Hivyo suala la kutumia bayoteknolojia kutengeneza.
” Hiyo ni teknolojia ambayo tunahitaji kujikita zaidi kama nchi ili tuweze kunufaika na hiyo teknolojia,” amesema.